Manispaa ya Morogoro yazindua mafunzo ya awamu ya pili zoezi la Uboreshaji daftari la wapiga kura.
Afisa MwandikishaAfisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini , Sheilla Lukuba, akifungua semina ya Mafunzo awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura leo Februali 30,2020. |
Afisa wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo akiwa katika semina.
ICTO , Frank Mwago akiendelea kutoa kutoa mafunzo kwa BVR na Waandikishaji katika Semina mafunzo ya awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura iliyofanyika leo Februali 30,2020. |
Maafisa Uchaguzi wa Manispaa ya Morogoro, wakiendelea kuelekezana jambo wakati wa semina. |
Baadhi ya Watendaji wa Kata wakifuatilia kwa umakini semina ya mafunzo ya awamu ya pili ya uboreshaji wa awamu ya pili ya Daftari la wapiga kura . |
HALMASHAURI ya
Manispaa ya Morogoro, imefungua rasmi mafunzo ya awamu ya pili ya Uboreshaji
wa Daftari la wapiga kura kwenye Ukumbi wa Mount Uluguru.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi
huo, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema
zoezi hili la awamu ya pili ya Uboreshwaji wa daftari la wapiga kura litawahusu
watu wote kwa maana ya kuandikishwa upya, kusahihisha taarifa pamoja na kufuta
taarifa.
Amesema zoezi zoezi
hilo LA Uboreshaji litaenda sambamba na zoezi la Uwekaji Wazi wa Daftari ambapo vituo vyote vya
kuandikisha Wapiga kura vitabandikwa Daftari ambapo wapiga kura watapaswa
kwenda kuhakiki Taarifa zao.
Aidha, amesema Zoezi la Uwekaji Wazi Daftari kuna njia
mbalimbali ambazo wapiga kura wanaweza kuzitumia mbali na kwenda Kituoni lakini pia wanaweza kuhakiki kwa njia ya Simu
(*152*00#) pamoja na kwenye Tovuti ya
Tume www.nec.go.tz .
“Tumefungua mafunzo yetu ya awamu ya pili ya uboreshaji
wa Daftari la wapiga kura, ni vyema
tukawashawishi Wananchi watumie njia hizi mbadala kama moja ya tahadhari hasa
katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa CORONA,nawaomba wananchi
wajitokeze kufanya maboresho na wale wasio jiandikisha waje lakini tahadhari
kubwa izingatiwe kama wanavyotoa wataalamu wa afya dhidi ya kujikinga na
ugonjwa huu wa CORONA –COVID 19 “ Amesema Lukuba.
Katika hatua nyingine ,Lukuba, amesisitiza kuweka tahadhari juu ya swala la
COVID-19 , Huku akisema kuwa ni Jukumu la TUME kutoa msisitizo wa kuepusha
misongamano vituoni nakutaka vituo vyote
viwe na nafasi ya kutosha.
“Ukimuona Simba anakuja huwezi ukakaa ukamwangalia hadi
anakuthuru lazima utumie njia za ziada za kukufanya asiweze kukudhuru na ndio
hivyo hivyo katika Kujikinga na Ugonjwa wa CORONA lazima uwe na jicho pana
zaidi na akili za ziada katika kujikinga lakini kubwa zaidi tujikinge sisis na
tuwakingine na wengine CORNA inaua” Ameongeza Lukuba.
Pia amevitaka Vituo vyote viwe na Ndoo zenye maji , sabuni
pamoja na Vitakasa Mikono ( Sanitizer) na kuwepo na muhudumu atakayekuwa
anafanya kazi ya kuangalia utaratibu wa foleni pamoja na kuhakikisha watu wote
wanaofika kituoni wananawa maji tiririka na sabuni kabla ya kuingia katika Vituo
nya Kujiandikisha.
Njia mbadala
zitakazotumika katika uhakiki wa daftari ni kama zifuatazo;
I.
Bonyeza *152*00#ok
II.
Chagua Namba 9 ambayo ni Uchaguzi Mkuu
III.
Chagua tena Namba 1 ambayo ni Uhakiki Taarifa za
Mpiga Kura
IV.
Baada ya hapo unatakiwa kuingiza Namba ya Mpiga
Kura (Utaweka Namba peke yake bila ya herufi
(T) wala , Dash (-)
Post a Comment