Header Ads

BODABODA Mazimbu wapongeza hatua za Diwani wao kuwapatia ndoo za maji na sabuni katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.


Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, (kulia), akimkabidhi kiongozi wa Kijiwe cha Bodaboda FK , kiasi cha Shilingi 30,000/= kwa jili ya kulipia faini kwa kosa la kutoweka ndoo ya maji katika kijiwe chao, lakini pia alikabidhi    ndoo ya Maji na sabuni.
Bodaboda wakipokea msaada wa Ndoo pamoja na sabuni kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga.



BODABODA Kata  ya Mazimbu, wamempongeza Diwani wa Kata hiyo , Mhe. Pascal Kihanga, kwa jitihada za kuwasaidia Ndoo  pamoja na  Sabuni kwa ajili ya kunawia  katika mapambano ya kujikinga dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa CORONA.

Wakizungumza kwa yakati tofauti tofauti, wamesema kitendo alichokifanya diwani wao ni cha kupongezwa kwani imeonyesha ni jinsi gani anavyowajali  Wananchi wake hususani katika kipindi hiki cha Janga la Ugonjwa wa CORONA.

Kwa upande wa Kiongozi wa kijiwe cha Maskani ya Bodaboda  Kitunda, Maneno Majaliwa, amempongeza Diwani wa Kata hiyo Mhe. Pascal Kihanga, lakini kubwa zaidi amesema wao hawatamuangusha na watahamasishana ili kuhakikisha kila Bodaboda anakuwa na Vitakasa mikono pamoja na kuweka Ndoo za Maji na sabuni katika Maskani zao ili kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

“Tuna mshukuru sana Mhe. Diwani wetu , Pascal Kihanga, kwa kweli amekuwa karibu sana na sisi katika kila jambo, Serikali imesema tusilete masihala , na sisi kama Bodaboda tutazitumia ndoo hizi vizuri na kuzitunza na tunamuhakikishia tutakuwa mabalozi wazuri kwa wenzetu katika kujikinga na Janga hili la Ugonjwa wa CORONA" Amesema  Majaliwa .

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kitunda Kata ya Mazimbu, Mhe. Henry Sebastian Mapunda,  amemshukuru Mhe. Kihanga huku akisema kuwa kitendo  alichokifanya Diwani wa Kata ya Mazimbu kinapaswa kuigwa na kuchukuliwa kama kiongozi aliyejitoa kwa ajili ya Wananchi wake.

"Tunamshukuru sana Diwani wetu, amekuwa akijitoa kwa mambo mbalimbali hata kwenye misiba na masherehe yetu amekuwa muhudhuriaji mkubwa sana na msaada kwetu, tuliona akitoa ndoo katika Makanisa na Misikiti lakini leo amewakumbuka Watoto zetu wa Bodaboda na amekuwa muhamasishaji mkubwa sana katika Ugonjwa huu , hivyo sisi tunaona hili ni jambo jema na sisi kama Wenyeviti katika Kata yake tutazidi kuendelea kuhamasisha  na kutoa elimu kwa Wananchi wetu  katika kujikinga na Janga  hili la Mlipuko wa Ugonjwa wa Homa kali ya mapafu CORONA"  Amesema Mapunda.




Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema kuwa lengo la kusambaza ndoo katika Vijiwe vya Bodaboda imetokana na maeneo hayo na Vijiwe vingi kutokuwa na ndoo jambo lililomfanya kuweza kuwasidia ili pesa zao wanazopata waweze kujikimu wao na familia zao.

Amesema katika utafiti wake amegundua kwamba asilimia kubwa ya Bodaboda hawajaelimika ipasavyo katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA, ambapo hali hiyo   ndiyo sababu iliyomsukuma kuelekeza ndoo katika maeneo hayo.


“Nimeona nielekeze nguvu na huku baada ya kuanza katika Nyumba za Ibada ikiwemo Misiki na Makanisa, nimeona  ni vyema nikapitia katika Vijiwe vilivyopo katika Kata yangu, japo sio vyote lakini malengo yangu ni kusambaza ndoo kwa Vijiwe vyote, tumeanza leo na zoezi hili litakuwa endelevu, lengo ni kuweza kuvipa nguvu Vijiwe hivi katika mapambano ya vita dhidi ya Ugonjwa wa CORONA ambapo katika  Vijiwe hivi  Vijana wetu asilimia kubwa wamekuwa wakitafuta ridhiki, tunaomba mvitunze vifaa hivi, isitokee mtu akaviiba tutamshughulikia , siwezi kuongoza Kata kama hakuna watu, jambo hili sio la kisiasa mkae mkijua, isije tokea wanasiasa wakawatenganisha katika jambo hili, bila nyie mimi nisingeongoza Kata, nategemea uhai wenu na afya zenu ili tuzidi kulifikisha Taifa hili mbele , tukiwa na Vijana wenye afya mbovu au tukikosa nguvu kazi kwa kuwapoteza hata maendeleo tutachelewa, ikitokea Mtu wa  CCM, CHADEMA , CUF na vyama vingine vya siasa  akawapa vifaa hivi tiba pokeeni lengo ni kuwafanya muwe salama nyinyi pamoja na familia zenu," Amesema Mhe. Kihanga.

Aidha, amewataka wananchi kutodharau ushauri wa Wataalamu badala yake waendelee kuchukua jitihada mahususi za kujikinga na Ugonjwa huo hadi pale mambo yatakapo kaa sawa na kama kuna mtu atajigundua ana viashiria vya Ugonjwa huo apige simu kwa wataalamu kama walivyotoa maelekezo ili hatua za awali ziweze kuchukuliwa.

Katika hatua nyengine, Mhe. Kihanga, amesema anatambua vipo Vijiwe vingi katika Kata yake vyenye uhitaji wa Ndoo pamoja na sabuni   lakini ameanza na Vijiwe vichache kisha atamalizia vijiwe vilivyobakia kwa awamu tofautitofauti lengoni kuhakikisha Wananchi wa Kata yake wanakuwa na uelewa mpana sana juu ya kujikinga na Ugonjwa CORONA pamoja na usalama wa afya zao.

Pia hakuishia katika Utoaji wa ndoo pekee, bali amechukua nafasi ya kuvitangaza Vitakasa mikono vilivyotengenezwa na Manispaa ya Morogoro na kuzinduliwa na Mkuu wa Wialaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo leo wakati wa uzinduzi wa Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Sabasaba iliyopewa jina la  Wodi ya Wazazi Regina Chonjo, huku akisema bei ya kitakasa mikono kimoja kitauzwa kwa Shilingi 2500/= na vinapatikana katika Idara ya Afya Manispaa ya Morogoro.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.