DC Chonjo akabidhi Jeshi la Polisi Wilaya ya Morogoro Barakoa 210 kwa ajili ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akipokea Barakoa kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya AEL mining Services , Ndg. Johan Austin , tukio hilo limefanyika Leo Aprili 30,2020 Ofisini kwake. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akimkabidhi Barakoa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Morogoro, OCD Jackson Kahamba. |
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Morogoro, OCD Jackson Kahamba, akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mdau aliyejitolea Barakoa hizo. |
Barakoa zilizotolewa leo na Kampuni ya AEL Mining Services kwa ajili ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Morogoro. |
Akizungumza na Waandishi wa
habari wakati wa kukabidhi Barakoa hizo,
Chonjo, amesema kuwa vifaa hivyo
vimetolewa na Kampuni inayojihusisha na upasuaji wa miamba ya Madini ya AEL Mining
Services iliyoko Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la kuwasaidia Jeshi la Polisi katika
kujikinga na maambukizi ya Virusi vya CORONA.
Chonjo,
amewahimiza Jeshi la Polisi kuendelea kuvaa Barakao wanapokuwa katika majukumu
yao ya kila siku kwani wao wamekuwa msaada mkubwa katika ulinzi wa Wananchi
pamoja na mali zao.
“Tumeitana
leo kwa lengo moja la kuwakabidhi Jeshi letu la Polisi Wilaya ya Morogoro,
wenzetu hawa wameamua kuliunga Mkono Jeshi la Polisi kwani wamekuwa wakiwaona
barabarani wakipamabana na uharifu na ulinzi wa raia na mali zao lakini wengine
wakiwa hawajavaa Barakoa jambo ambalo limewagusa na kuona ipo haja ya kujitolea
Barakoa hizi kuwakinga Askari wetu dhidi ya Janga hili la ugonjwa wa CORONA
ambalo hatari kwa maisha ya Binadamu” Amesema DC Chonjo.
Kwa upande wake Kamanda wa
Polisi Wilaya ya Morogoro (OCD ) Jackson
Kahamba, amemshukuru DC Chonjo, kwa kuwaletea mdau ambaye amewakabidhi sialaha
bora katika kujikinga na Uginjwa wa CORONA.
OCD Kahamba, amesema DC
Chonjo, amekuwa mstari wa Mbele katika maendeleo ya Wilaya hususani katika
Jeshi la Polisi na familia zao lakini kubwa amekuwa akiwasaidia Wananchi wake
kwa kila jambo linapotokea huku akiwahimiza viongozi wengine kuiga mfano wa DC
Chonjo kujitolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
“Tunampongeza sana Mama yetu
Chonjo, amekuwa mlezi bora sana kwa upande wetu wa Jeshi la Polisi akiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya amejitoa sana kwetu na familia
zetu, hivi karibuni alitoa msaada wa Shilingi Milioni 1 kwa taaisisi ya Mama
Mutafungwa inayosaidia kujikwamua kiuchumi kwa wakina mama wanaoishi katika Nyumba za Polisi kwa kweli
amekuwa akijitoa sana na anafanya kazi kubwa sana kipindi hiki kuhakikisha
wananchi wa Wilaya yake wanakuwa salama kwa kujikinga na virusi vya Corona”
Amesema OCD Kahamba.
Naye Mkurugenzi wa AEL Mining Services , Ndg. Johan
Austin,amesema wameamua kutoa Barakoa kwa Jeshi la Polisi baada ya kuona Askari
wengi wapo mitaani wakipambana na maisha ya Wananchi lakini wengi wao hawana
Barakao jambo linalipolekea kuhatarisha maisha yao.
“Leo
tumekabidhi Barakoa 210 kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ili awakabidhi Jeshi la
Polisi Wilaya yake, tumeona jitihada za DC wetu katika Janga hili sisi kwa
upande wetu tukaona ni vyema tukajikita kulisadia Jeshi la Polisi kwani wamekuwa
msaada mkubwa katika ulinzi wa wetu na mali zetu kwa ujumla, hawa wanapambana
na waharifu, ujambazi kwahiyo lazima wawe wamejikinga hususani katika
kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa CORONA” Amesema Austin.
Amesema
Polisi wengi kazi zao wanazifanya kwenye mikusanyiko , hivyo kwa Barakao
walizokabidhi zitasaidia kujikinga katika maeneo yenye mikusanyiko na maeneo maalum kama
ofisini, kwenye malindo pamoja na sehemu za kuabudia.
Post a Comment