Manispaa Morogoro yatenga Kituo cha huduma Afya Stendi ya Msamvu kwa washukiwa wa CORONA.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imetenga Kituo cha kutolea huduma Afya katika Stendi ya Mabasi Msamvu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Mganga Mkuu Wa Manispaa Morogoro, Dr. Ikaji Rashid, amesema lengo kuweka Kituo hicho ni kusaidia kutoa huduma kwa mtu yeyote mwenyekujihisi na dalili za ugonjwa Wa Corona au anayeshukiwa kuwa na ugonjwa huo.
Aidha, amesema kumekuwa na Changamoto ya baadhi ya watu wanaoshukiwa na ugonjwa Wa Corona kuhisiwa tofauti na kupelekea usumbufu Wa baadhi ya Magari kuchukua muda mrefu kumpeleka mshukiwa huyo Hospitali .
" Juzi tulipokea taarifa kwamba kuna gari lilimpeleka mshukiwa Wa ugonjwa Wa corona huku Gari hilo likiwa lina abiria na kusindikizwa na king'ora jambo ambalo lilileta taharuki kwa wananchi , kwahiyo ili kudhibiti hali hii tumeona kuwasogezea huduma karibu ili anaye jihisi au mshukiwa afikishwe hapo na kupatiwa huduma ya kwanza " Amesema Dr. Ikaji.
Amesema wamefanya hivyo kwakuwa eneo hilo lina mikusanyiko ya watu mbalimbalj ikiwamo wafanyabiashara, pamoja na wasafiri.
Hata hivyo amewataka Mawakala Wa mabasi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu Wa Afya na Viongozi Wa ngazi za juu katika mapambano ya virusi vya Corona na kuhakikisha kila Gari linakuwa na ndoo za kunawia Maji , sabuni pamoja na vitakasa mikono.
Pia amesema zinaandaliwa fomu kwa ajili ya Ukaguzi Wa upuliziaji Wa Magari yote yanayoingia na kutoka katika Stendi ya Msamvu.
*CORONA INAUA CHUKUA TAHADHARI*
Post a Comment