Header Ads

RC SANARE APOKEA MSAADA WA MABATI 100 KUTOKA KANISA LA FAITH BAPTISTA CHURCH KWA AJILI YA UKARABATI WAUJENZI WA SHULE YA MSINGI MJI MKUU MANISPAA YA MOROGORO.






Mchungaji wa Kanisa la Faith Baptist Church lilopo Kola "B" , Mchungaji Jerry Max Wyatt (kulia) akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare.


Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mhe. Loata Sanare , Katibu Tawala Mkoa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo na mafundi wakisaidia kupandisha Kenchi katika ujenzi wa madarasa ya Shule ya Misngi Mji Mkuu.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare akitoa hotuba fupi kabla ya kupokea msaada wa mabati.









MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare amepokea msaada wa bati 100 zenye ubora wa Geji 28 kutoka Kanisa la Faith Baptist Church  kwa ajili ya kuwezesha huduma ya ukarabati wa Ujenzi wa Shule ya Msingi Mji Mkuu iliyopo Manispaa ya Morogoro.


Mara baada ya kukabidhiwa msaada huo nje ya Jengo la Shule hiyo, Sanare alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina  Chonjo , Mabati 100 ambapo katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo, , Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Eng. Joyce Baravuga , Mku wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, Katibu Tawala Morogoro, Ruth John, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Afisa Elimu Manispaa ya Morogoro pamoja na Watumishi wa Manispaa na Walimu wa Shule hiyo. 

Amesema kuwa msaada huo utasaidia kuezekea Mapaa ya Madarasa yanayoendelea kukarabatiwa na kupelekea miundombinu ya Shule hiyo kuimarika kutokana na uchakavu wa Vyumba vya mdarasa yalipo kwa sasa.

Aidha, amesmhukuru Mchungaji wa Kanisa la Faith Baptist Church lilopo Kola "B" , Mchungaji Jerry Max Wyatt kwa msaada alioutoa kama sehemu ya kusaidia  Jamii ya Manispaa ya Morogoro ili kuendelea kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa kwa kuchangia huduma za maendeleo hususani katika Sekta ya Elimu.

"Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mchungaji, Jerry Max , kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Sekta ya elimu katika Manispaa yetu ya Morogoro naahidi tutatumia ipasavyo katika kuleta maendeleo ili kuweza kupunguza changamoto mbalimbali katika Sekta ya elimu, tangia tuanzishe Kampeni zetu za kuchangia masuala ya elimu, tumepata wadau mbalimbali waliotuunga mkono, tumeanza na vyumba 8 lakini tutaendelea kupanua wigo ili kuongeza ukarabati wa ujenzi wa vyumba vingine 9 vilivypobakia , lengo nataka Shule hii iwe ya mfano kwani ipo katikati ya Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ni jambo la aibu Shule hii kutoifanyia ukaarabati harafu ipo njia kila nikipita naiona na Viongozi wa Kitaifa wanapita hapa hapa, tunawepongeza wadau wote tukianza na Nashela Hotel, Wamachinga, Wauza mbao pamoja hawa ndugu zetu wa Kanisa" Amesema RC Sanare.

Aidha, amesema kuwa sio kila wakati tuwe tegemezi kwa Mataifa ya nje, lazima wananchi waonyeshe uzalendo wa kuchangia maendeleo katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo hususani katika Sekta ya Elimu ambayo Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli alishatoa tamko la Elimu bure bila malipo.

Hata hivyo, amesema wakati Taifa likiwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa CORONA, basi nguvu nyengine zielekezwe katika kupambana na maendeleo.

Pia ameendelea kusisitiza kwamba wale walimu Wakuu waliodumu muda mrefu bila ya matokeo mazuri ya ufaulu watashushwa vyeo na kuwa walimu wa kawaida.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo, amesema moja ya mipango ya mkoa katika uboreshaji wa Sekta ya Elimu ni pamoja na kuimarisha Uongozi wa Shule pamoja na Kamati zake ili ziendelee kuwa hai na kupata matokeo chanya katika ufaulu wa wanafunzi na kukuza Sekta ya Elimu.


"Tunawashukuru sana wadau katika kuchangia maendeleo ya elimu, lakini kuna vitu vinawezwa kufanya na jamii katika maendeleo ya Sekta ya elimu, kwahiyo yale yaliyo katika uwezo wa kufanywa na Jamii yafanywe na yale ambayo yapo nje ya uwezo wao waiachie Serikali iweze kupambana nayo"Amesema Kalobelo.

Aidha , amesema kuwa ili mfumo wa elimu uweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kuleta maendeleo cnaya katika Sekta ya elimu lazima miundombinu iwe ya kuvutia na kuimarisha miundombinu yote kuanzia ngazi ya elimu msingi na Sekondari.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Regina Chonjo, ametoa pongezi kwa wadau wanaoendelea kuchangia maendeleo ya Sekta ya Elimu huku akiwataka Wazazi nao kuwajibika kwani wao ndio wenye watoto wanaosoma katika shule hizo.




"Maendeleo katika jamii yanaletwa kwa ushirikiano kati ya serikali  na wananchi kwa kusaidiwa na wadau mbalimbali  katika kufanikisha mahitaji muhimu, hivyo nawapongeza wadau wote waliofanikisha kwa namna moja au nyengine katika kuchangia maendeleo katika mbalimbali za maendeleo hususani katika ukarabati huu wa Shule yetu iliyokuwa na Majengo chakavu na leo Wanafunzi wetu wakirudi Shuleni watasoma katika mazingira rafiki na kuongeza viwango vya ufaulu" Amesema DC Chonjo.


Katika hatua nyengine, DC Chonjo, amewataka waalimu na watendaji kuhakikisha kila mtu anafanya majukumu kwa nafasi yake huku akiwataka watendaji pamoja na maafisa elimu kuhakikisha kila kinachoingia na kutoka wakisimamie kwa misingi ya sheria na kanuni.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amepongeza mkuu  wa Mkoa, Mhe. Loata Sanare , Mkuu wa Wilaya ya  Morogoro, Mhe. Regina Chonjo   kwa kuunganisha  wadau  mbalimbali  katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuahidikutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa wa madarsa mengine yaliyobakia.


‘Tunaushukuru sana Uongozi wa Mkoa, Wilaya na  Wadau wa maendeleo  kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutayatumia Mabati haya kama mlivyokusudia katika ukarabati wa madarasa ya shule hii, lakini maagizo yaliyotolewa na Mkuu wetu wa Mkoa na wa Wilaya tutayafanyia kazi, tunaahidi tutakwenda kukaa na wananchi wetu na tutachangisha pesa ili tuendeleze maendeleo ya elimu " Amesema Lukuba.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mji Muu, Bi. Grace Malya, ameushukuru Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa , pamoja na Wadau wa Maendeleo huku akisema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyokusudiwa.

Amesema  shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa Ofisi ya Walimu  hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

Naye , Mchungaji wa Kanisa la  Faith Baptist Church ,Mchungaji Jerry Max Wyatt, amesema msaada huo ni pamoja na kuhakikisha Sekta ya elimu katika Manispaa ya Morogoro inakuwa kwa kasi .


"Tumeamua kutoa msaada huu kutokana na kuguswa na masuala mazima ya maendeleo katika Manispaa ya Morogoro, tulikuwa tunamuona Mkuu wa Mkoa akihangaika kutafuta wadau nasi tukaona tumuunge mkono kwa hiki tulichokitoa lengo ni kuonyesha hatupo katika masuala ya kiroh pekee bali tupo katika kuona masuala mbalimbali ya maendeleo yanapiga hatua na tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kile tutakachojaliwa nacho" Amesema Mchungaji Max.



























No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.