KISHINDO CHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATA YA MAFISA MANISPAA YA MOROGORO KIPINDI CHA MIAKA 4 YA JPM.
Kituo cha Afya Kata ya Mafisa. |
Kitanda kilichokabidhiwa katika Kituo cha Afya hicho chini ya ufadhili wa Benki ya NMB. |
Mhe. Diwani wa Kata ya Mafisa , Mhe. Daudi Mnadi akionyesha Kitanda na chumba cha Wagonjwa ambapo mwezi huu wa Nne huduma ya Mama na Mtoto itaanza kutolewa katika Kituo hicho cha Afya. |
Muonekano wa ndani wa Kituo cha Afya cha Mafisa. |
Mhe. Diwani wa Kata ya Mafisa, Daudi Mnadi (kushoto) akiwa na Mtendaji wake wa Kata wakionyesha baadhi ya Vifaa vilivyokabidhiwa kwa ajili ya kutolea huduma. |
Viti kwa ajili ya Wagonjwa.
Jengo la Utawala Shule ya Sekondari Kayenzi. |
Vyumba 2 vya Madarasa vilivyojengwa kwa fedha za Serikali Kuu katika Shule ya Sekondari Kayenzi. |
Jengo la Maabara linaloendelea na Ujenzi katika Shule ya Sekondari Kayenzi. |
Vyumba 3 vya Madarasa katika Shule ya Msingi Muungano ambavyo vilijengwa kwa fedha za vyanzo vya ndani vya Manispaa pamoja na chumba kimoja chini ya Ufadhili wa Kiwanda cha 21th Century Polister . |
Ujenzi
wa Madarasa 2 mapya ya Shule ya Msingi Muungano yakiendelea na Ujenzi kupitia fedha za mapato ya ndani ya Manispaa .
|
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akikagua Shuka zilizotolewa na Wafadhili kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya kutumika katika Kituo cha Afya Kata ya Mafisa. |
KATA ya Mafisa ni miongoni mwa Kata 29 zinazopatikana katika
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Kata hiyo inaongozwa na Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi CCM
, Chini ya Diwani, Mhe. Daudi Salum Mnadi, ambapo katika kipindi cha Miaka 4
Chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dtk. John Pombe Magufuli yapo mengi yamefanyika katika kutekeleza Ilani ya CCM
ya Mwaka 2015 ikiwamo huduma za Afya, Miundombinu, Elimu pamoja na Michezo.
Katika mazungumzo na Mhe. Diwani wa Kata ya Mafisa, Mhe.
Daudi Mnadi, amesema kuwa tangia aingie madarakani mwaka
2015, kuna miradi ilikuwa haijatekelezwa lakini kwa
jitihada zake yapo mambo mbalimbali ameyafanya nakuleta maendeleo katika Kata
hiyo.
Amesema miradi ya
maendeleo walioifanya na Uongozi wake wa Kata imeonyesha dhahiri kwamba Ilani
ya CCM imetekelezwa kwa mafanikio makubwa sana na kuthibitisha jinsi ambavyo
Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt John Magufuli
inavyowaletea Wananchi Maendeleo ya uhakika kwenye Kata ya Mafisa, Mkoa wa
Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
Katika ngazi ya Elimu,
Mhe. Daudi amesema Kata ya Mafisa ina
Shule mbili ambapo kati ya shule hizo , moja ni Shule ya Sekondari Kayenzi
pamoja na Shule ya Msingi Muungano.
Hakuishia katika jitihada
zake mwenyewe, lakini amesema kwa
kutambua na kuthamini kazi kubwa
zinazofanywa na Ofisi ya Afisa Mtendaji , amehamasisha na kusimamia ukarabati
wa Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Kayenzi ambapo awali Walimu
walikuwa wakitumia vyumba vya Madarasa lakini kukamilika kwa Jengo hilo
kumeokoa jumla ya Vyumba 4 vya Madasara na sasa uhaba wa Madarasa Kata ya Mafisa
kwa upande wa Shule ya Sekondari hakuna tena.
Ujenzi huo wa Jengo la
Utawala umetumia jumla ya Shilingi Milioni 17,ambapo Serikali Kuu ilitoa
Shilingi Milioni 15 na Manispaa ya Morogoro ilichangia Shilingi Milioni 2 kwa kununua Samani
huku Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, akichangia jumla
ya Shilingi 1,800,000/=.
Hakuishia katika Ujenzi wa
Jengo la Utawala pekee, bali katika kuboresha elimu Kata hiyo iliingiziwa kiasi
cha fedha chenye thamani ya Shilingi Milioni 25 kutoka Serikali Kuu kwa ajili
ya Ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa, na Madarasa hayo yameshaanza kutumika.
Pia katika upande huo wa
Elimu Sekondari, kwa Sasa Kata ya Mafisa ipo katika hatua za Mwisho kukamilisha
Maabara ya Shule ya Sekondari Kayenzi, ambapo baada ya kukamilika kwa Maabara
hiyo watakuwa na Ongezeko la Madarasa 11 huku akidai kwamba uhaba wa Madarasa
kwa upande wa Elimu Sekondari hakuna tena na watakuwa na uwezo wa kupokea
Wanafunzi wengi bila changamoto yoyote.
Kwa upande wa Shule ya
Msingi Muungano, Mhe. Daudi, amesema kuwa awali Shule hiyo ilikuwa na
changamoto ya Madarasa lakini ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa
kuwapatia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 2 vya
Madarasa yaliyokamilika na tayari
wanafunzi wameshaanza kuyatumia pamoja na nguvu ya Wananchi ambao kila mmoja
aliweza kushiriki kwa kutoa fedha na wengine kuchangia vifaa kama vile Matofali
na mifuko ya Saruji.
Amesema Vyumba 2 vya
Madarasa vinavyoendelea kwa sasa ambavyo bado havijakamilika, vimetokana na nguvu
ya Wananchi kuanzia kwenye vifaa pamoja na Matofali huku Manispaa ikiwaingizia
Shilingi Milioni 25 ambapo hatua iliyobakia ni ya upauaji.
Pia ameupongeza Uongozi wa
Kiwanda cha Mohammed Enterprises cha 21 th Century Textile Ltd Polyster kilichopo kwa kuwasaidia katika
Ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa kwa kuwapatia Shilingi Milioni 14 na
ukamlihsji wa chumba hicho ulitokana na nguvu ya Wananchi.
Hivyo kwa sasa Shule hiyo
ya Msingi ya Muungano haina tena upungufu wa Madarasa kwani hadi kukamilika kwa
Madarasa 2 yaliyobakia itakuwa na Maboma 5 ambapo itamudu uwezo wa kuwapokea
Wanafunzi wengine wapya ifikapo mwakani ambapo kwa sasa changamoto iliyokuwepo
ni uhaba wa matundu ya Vyoo katika upande wa Sekondari na Msingi.
Kuhusu Sekta ya Afya,
Chini ya Uongozi wa Mhe. Daudi Salum Mnadi,Kata ya Mafisa haikuwa na Kituo cha Afya takribani miaka 17
sasa lakini kwa sasa tayari wameshaanza
ujenzi na ametoa shukrani kubwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa
kufufua matumaini ya kuwa na Kituo cha Afya kikubwa kuliko vyote katika Manispaa
ya Morogoro ambapo Kituo hicho kinatarajia kutoa huduma za Mama na Mtoto
kuanzia mwezi Aprili 2020.
Amesema mpaka sasa Ujenzi wa baadhi ya Vyumba ikiwemo vyumba
vya huduma na Ofisi tayari vimeshakamilika na vipo tayari kwa utoaji wa huduma.
Miongoni mwa vitu vilivyo katika Kituo hicho cha afya ni
pamoja na Vitanda vya kuwalazia Wagonjwa, Kitanda cha Chumba Upasuaji, Vifaa
vya Huduma ya Kwanza , Mashuka 15 na Vitanda 5 ambavyo vyote vimefadhiliwa na
Benki ya NMB pamoja na Mashine ya kupima uzito kwa Watoto.
Lakini kwa upande wa thamani zipo , Viti 10 kwa ajili ya
Wagonjwa , Viti 5 vya Ofisi , meza 4
ndogo za Ofisi pamoja na meza kubwa moja kwa ajili ya huduma ya Mama na Mtoto
vyote vilinunuliwa kwa fedha ya Manispaa .
Aidha, Mhe. Daudi, hakuacha mbali Sekta ya Miundombinu ambapo
ametekeleza upanuaji wa kuichonga Barabara inayoingia Sina kuelekea Shule ya
Sekondari Kayenzi mwaka 2015 ambapo ilikuwa haipitiki vizuri.
Kwa upande wa Ulinzi na
Usalama, ameendelea kushirikiana na Uongozi wa Serikali za Mitaa na Kata
kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarishwa katika maeneo yote ambapo kwa kushirikiana
na Mtendaji wa Kata na Baraza la Maendeleo la Kata wamehakikisha Kata inakuwa
salama wakati wowote kwa maendeleo ya Wananchi na ulinzi wa mali zao.
Hata hivyo amechukua
nafasi ya kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli, kwa jitihada za kukamilisha miradi ya Kimkakati hapa nchini lakini
ameupongeza sana Uongozi wa Manispaa ya Morogoro chini ya Mkurugenzi wa
Manispaa, Sheilla Lukuba, kwa kumuingizia fedha za miradi katika Kata yake
pamoja na kulishukuru Baraza la Madiwani chini ya Mwenyekiti Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, kwa kazi nzuri wanayoifanya katika
Maendeleo ya Manispaa ya Morogoro na utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya
Kimkakati.
Post a Comment