Mkurugenzi Manispaa Morogoro afufua matumani ya Mradi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa umakini vifungu vya kikao.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,
amewataka Wananchi wa Manispaa ya
Morogoro kuondoa hofu juu ya Mradi wa Stendi ya Daladala Kaloleni baada ya kusimama kwa muda mrefu kufuatia Mkandarasi kuukacha mradi huo .
Hayo ameyazungumza leo Februali 30, katika kikao cha
Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya
Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Lukuba, amesema
matumaini ya Ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni yamefufuka kufuatia kupata
Mkandarasi Mpya kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra ambayo ndiyo inayoendelea na Ujenzi wa
Soko Kuu la Kisasa na Stendi mpya ya Daladla Mafiga.
Aidha, amesema kwa
sasa Mkandarasi yupo eneo la tukioa na tayari ameshaanza kazi ambapo katika
kandarasi yake amepewa muda wa miezi 2 sawa na siku 60 ili kukamilisha Ujenzi
wa Stendi hiyo.
Lukuba amesema Ujenzi
huo utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 640 ambazo ni fedha za mkopo wa Benki
ya Dunia chini ya fedha za uboreshaji Miji ( Urban Local Government
Strengthening Program (ULGSP) .
“Tunaishukuru sana
Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutupatia fedha za miradi mingine, ametupatia
fedha za Mradi wa Soko Kuu la Kisasa Bilioni 17 , Stendi ya Daladala Mafiga
Bilioni 5.2 , Mto Kikundi ukarabati
jumla ya Milioni 774, Shule ya Sekondari Mji Mpya Bilioni 1.4, ukarabati wa
Shule Kongwe ya Sekondari Morogoro na
miradi kibao , tunakila sababu ya Kumpongeza kwani atatufanya Manispaa kuweza
kukusanya na kuongeza mapato yetu ya ndani bila kutegemea Serikali kuu “ Amesema Lukuba.
Amesema kufuatia
kuvunja mkataba na Kampuni ya Fast iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa Stendi ya
Kaloleni, tayari ameshaunda Tume itakayochunguza gharama zilizotumika na
kampuni ndipo waweze kuwafungulia mashataka ya madeni yaliyobakia.
Amesema Kampuni ya
Fast ilichukua mkataba wa muda wa miezi 3 sawa na siku 90 ambapo walipewa kiasi cha Shilingi Milioni
108 lakini walishindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati licha ya Kuongezewa muda
wa siku 45 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo
kufuatia kuukacha mradi huo na kutokomea.
Katika hatua nyeninge, Baraza la Madiwani la Manispaa
ya Morogoro, limeomba kujua pesa halisi zilizotumika katika Ujenzi wa Stendi ya
Mafiga na taarifa zake zifikishwe katika Kikao cha Kamati ya fedha kijacho ili
kama kuna fedha zimebakia ziweze kutumika katika ujenzi wa Vioski vya Biashara
pamoja na Mabanda ya Mama na Baba lishe ikiwemo na maeneo ya Wamachinga.
Post a Comment