Header Ads

Mchungaji Mashimo amtaka Diamond kufanya ibada kama anahitaji kufika mbali zaidi.





MCHUNGAJI wa Manabii na Mitume Tanzania, Daudi Mashimo, amemtaka Msanii Maarufu wa Bongo Fleva, Naseeb Abduly maarufu kama Diamond kuanza kufanya ibada kama anahitaji kufika mbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo  Julai 28/2019 Kinondoni, amesema vita inayomuandama Diamond ni kubwa sana asipo jipanga itamfikisha pabaya.


Amesema kuwa Vitu  vinavyomsaidia ni pamoja na kujitoa katika Jamii pamoja na kutoa misaada mbali mbali kwa Jamii.


Aidha amesema kutokana na jitihada zake za kusaidia Jamii kuna vita kubwa sana dhidi yake.

 Amesema ipo  vita na kuna baadhi ya watu wamejipanga kuisambaratisha familia ya Diamond.

Amesema kwa maono yake ya unabii atafanya mkesha  maalumu Tarehe 5 Juni  2019 wa kumuombea ili vita aliyokuwa nayo  na maadui zake anaisambaratisha.


Amesema kama Diamond asingekuwa anasaidia Jamii na kutokuishi vizuri na wapo asingefika hapa alipo.


 " Diamond ndugu yangu, Fanya ibada na weka utaratibu wa kuombea mimba ya mpenzi wako na uachane na zinaa utafika mbali zaidi" Amesema Mchungaji Mashimo.

Amesema ndoa halisi ya mke  ambaye Diamond atadumu nae itafanyika 2020.


Pia amewataka wale wanaomtukana waendelee kumtukana ila yeye anachanja mbuga.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.