DC Mjema awataka Wahitimu kidato cha Sita Shule ya Sekondari Al Muntazir kuwa wazalendo katika kulipa Taifa Maendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanapoenda wanaweka Uzalendo mbele ili kulitumikia Taifa.
Hayo ameyasema Leo kwenye mahafali ya kuwaaga wanafunzi hao yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa King Solomon Jijini Dar Es salaam.
Amesema ili Taifa lipige hatua linataka Vijana wasomi na kwenye moyo wa kizalendo kwani anaamini Vijana hao watatimza maagizo yake.
Amesema Rais Dkt John Magufuli ameweka Mazingira mazuri ya elimu baada ya kutangaza Elimu bure ili kila Mtoto asome hususani kwa Watoto wa Wanyonge na Masikini.
Amesema kuwa wapo watakao kwenda vyuo vikuu moja kwa moja na wapo watakaojiunga na vyuo vya kati hivyo wazingatie uzalendo na wasipotoshwe kwani elimu ya juu ina changamoto nyingi sana.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kukuza elimu hapa nchini, kwani Rais Dkt John Magufuli ametoa elimu bure ili kila Mtanzania asome.
Aidha amesema Tanzania ina rasilimali nyingi hivyo ni lazima wataalamu watoke hapa ili tunufaike na kufikia malengo katika kuelekea uchumi wa Kati.
Pia amewataka waalimu kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutunza Mazingira kwani sasa magonjwa ya milipuko yamekua changamoto hivyo lazima wawe wasafi.
" Tuna kipindu pindu na Dengue , hii inatokana na uchafu lakini zaidi sisi tunachangia kutupa taka taka Hivyo, niwaombe muwafumdishe watoto ili wawe mabalozi wazuri katika Jamii zetu".
Katika hitimisho, amempongeza Rais Dkt John Magufuli , kwa uchapakazi na kuweka Mazingira mazuri ya Wawekezaji kuelekea uchumi wa Kati na Tanzania ya Viwanda.
Post a Comment