Header Ads

Kaimu Meya Ilala afungua Kongamano la Vijana juu ya Elimu ya Ujasiriamali lililoandaliwa na Vijana House Vision.




 KAIMU Meya Ilala, Mh Omary Kumbilamoto, amefungua kongamano kongamano la  Vijana LA ujasiriamali lililofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es salaam leo Julai 22 mwaka 2019.

 Kongamano hilo  limeandaliwa na Taasisi ya  Vijana House Vision lenye makazi yake Kijitonyama.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo, Mh Kumbilamoto , amesema kuwa watu waliotajirika na wenye  uchumi mkubwa ni wale waliojiajiri na wafanya Biashara wakubwa.

 Amesema Serikali ya awamu ya tano ipo  kwa ajili ya kuwakwamua wanyonge na masikini ili kufikia uchumi Wa kati.

 Amesema Serikali ya awamu ya tano  imetenga 10% kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha kiuchumi wakina mama , Vijana na walemavu.

Amesema wapo baadhi ya madiwani wamekuwa wakwamishaji katika kuwasainia vikundi hivyo kama kutatokea changamoto hizo waziwasilishe kwa Wakurugenzi wao watachukua hatua.

 Amesema wapo baadhi ya watendaji na Viongozi wamefikisha nchi hapa tulipo lakini Rais Dkt John Magufuli anapambana na hatimaye Maendeleo yanaanza kuonekana.

 Pia amesema wanatarajia Manispaa ya Ilala kuwa na vivutio vya utalii ikiwamo pamoja na Uwanja wa Mnazi Mmoja uwanja wa Mashujaa kwa kutoa ajira ya zaidi ya watu 1000 hivyo ni fursa kwa vijana kuzifanyia kazi na kufanya ilala inapata kitega uchumi na chanzo cha mapato kwa Maendeleo ya Taifa.


" Nataka kuwaambia msibweteke changamkieni fursa hizi Rais wetu anatupenda hivyo lazima tufanye kazi kwa Maendeleo ya kweli" Amesema Kumbilamoto.

 Naye Mkurugenzi wa Vijana House Vision, Peter Mayunga, amemshukuru mgeni rasmi na kumpongeza pamoja na Manispaa ya Ilala ikiwamo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema kwa kazi anayoifanya.


Pia amesema Vijana House Vision imetenga Hekari 50 za kilimo cha Matikiti Chalinze pamoja na Hekari 20 kwa ajili ya kilimo cha Mpunga.

 Hivyo amewataka Vijana kuchangamkia fursa kujikwamua kiuchumi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.