Mkurugenzi ilala awatangazia kiama wakwepa kodi ifikapo Julai 1 Mwaka huu.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, amesema kuanzia Leo atafanya msako kwa wafanya Biashara wasio na leseni katika Manispaa ya Ilala. Hayo ameyasema Leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Katika Ukumbi wa Anautoglo Jijini Dar Es Salaam..
Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema msako huo unaanza baada ya kuwepo na wafanya Biashara zaidi ya 10000 wasio lipa kodi ambao wamesababisha kutofikia malengo ya ukusanyaji wa Mapato waliyojiwekea.
Amesema mpaka sasa wamekusanya jumla ya Bilioni 52 sawa na 92% ambapo ni tofauti na lengo walilojiwekea la kukusanya Bilioni 56. Amesema Manispaa ya Ilala inakadiriwa kuwa na wafanya Biashara 332900 lakini walolipa kodi ni wafanya Biashara 23328.
Aidha amesema Kariakoo inawafanya Biashara 13125 lakini waliokuwa na leseni ni wafanya Biashara 8671.
Amesema Kata ya Jangwani inawafanya Biashara 957 lakini cha kushangaza wenye leseni ni wafanya Biashara 655 na wasio na leseni ni 302.
Pia amesema eneo jengine ambalo lilikuwa na shida ya ukusanyaji kodi ni Nyumba za kulala ikiwamo Gesti na Hoteli ambapo ukusanyaji kodi wake hauridhishi.
Pia amesema kuwa upande wa Majengo nako ukusanyaji kodi wake hauridhishi , kwani walipanga kukusanya kiasi cha Shilingi Billioni 7 lakini mpaka sasa wamekusanya Milioni 400.
Pia amefafanua kwamba ushuru wa Kuzingira kwa majengo makubwa na kodi za ushuru wa huduma wamefanya vizuri japo haukuridhisha sana.
Amesema malengo ya kodi za huduma ilikuwa kukusanya Bilioni 17 lakini sasa wanakaribia 100% ya kukusanya kodi Hiyo.
Amesema Bilioni 3 zimeshatumika katika kujenga vyumba vya madarasa ambapo vyumba 127 vimejengwa na jumla ya Shilingi Bilioni 1 zimepelekwa shule za Msingi.
Miongoni Mwa shule hizo ni pamoja na Kinyerezi, Ulongoni, Savara.Pia wamefanikiwa kujenga shule mpya za Sekondari kama vile, Mivinjeni, Buguruni, Kisuru na Shule ya Uamuzi na Kinyerezi lengo ni watoto wote watakaofaulu mwakani waende shuleni.
" Lazima tulipe kodi, kodi hizi ndizo zinapelekea kukamilisha miradi ya Maendeleo, hata Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli amesisitizia Kodi hivyo lazima tutekeleze hili jambo kuweza kifikia uchumi wa kati " Amesema Mkurugenzi Shauri.
Mbali na hayo amesema kuwa mpaka sasa wamewawezesha wakina mama , Walemavu na Vijana katika kuwapatia mikopo hivyo Tarehe 24 wanaenda kutoa tena mikopo ya Boda boda 30, Bajaji 50, Gari aina ya Costa na IST moja na fedha taslimu Bilioni 2.
Amesema suala la Machinjio limekamilika washaingia mkataba na NHC.
Amesema katika Operesheni ya siku 13 itakayoanza leo hakuna faini lakini kuanzia Tarehe 1 Julai 2019 asiye na leseni faini Laki moja hadi Milioni.
Amesema katika kuwarahisishia malipo ya kodi wameweka kituo Buguruni kwa watu wa mbali bila kufika anautoglo
Post a Comment