Header Ads

Katibu Tawala Wilaya ya Ilala amewataka Wanafunzi wasome kwa bidii ili waje kuwa na maisha mazuri.







Katibu Tawala Wilaya ya Ilala amewataka Wanafunzi wasome kwa bidii ili waje kuwa na maisha mazuri.


Hayo ameyasema leo  wakati akimwakilisha Mkuu Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, kwenye kokangamano la  kumkomboa mtoto Wa kike  dhidi ya maisha hatarishi katika kupata elimu.


Kongamano hilo limefanyika kimkoa Wa Dar Es Salaam kwenye Shule ya Sekondari Jangwani, ambapo jumla ya Shule 64 zimeshiriki na kuwatoa wawakilishi.

 Amesema Mtoto Wa kike  anachangamoto nyingi Hivyo ameishukuru COMFED ( Campaign For Female Education) kwa kujitoa kwao.


Amesema Serikali ya awamu ya tano  imetoa elimu bure Hivyo kila mtu  lazima asome na kuitumia nafasi hiyo  adhimu kutoka kwa Rai Dkt John Magufuli.

 " Kataeni bebies mnatakiwa msome ili tuwapate wakina Mama Samia , Mama Mjema na wengine, mkiishiwa kudanganywa mtafeli na maisha yenu yatakuwa magumu, achaneni na Mababa ya mjini yakiwaita mwambie ujana wako umekula wapi na uzee umalizie kwangu sawaaa" Amesema DAS.

 Pia amefikisha salama za Mkuu Wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema,  akiwaambia anawapenda sana angependa kujumuika nao lakini amepata majukumu mengine ya Kitaifa.


Naye  Mjumbe Wa Kamati ya CDC " Comfed District Committee) na Afisa Ustawi Wa jamii Manispaa ya Kigamboni, Bibi Grace Msofu,ameupongeza Uongozi Wa Wilaya ya ilala ikiwamo DC Mjema kwa kuwa karibu na Jamii.

Amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuwasaidia wasichana katika elimu kwa kutoa Vifaa vya shule kwa watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu au hatarishi walio katika Shule za Sekondari.


Aidha, Afisa Habari na Mahusiano Manispaa ya Ilala na aliyekuja kwaniaba ya Mkurugenzi , Tabu Shaibu , amewataka Watoto hao kutojihusisha na makundi hatarishi kama wanataka kufaulu mitihani yao.

Amesema wao kama Manispaa wapp tayari kushirikiana na COMFED kwa Maendeleo ya elimu Wilaya ya Ilala, ngazi y mkoa hadi Taifa.
Miongoni mwa Mataifa ambayo COMFED inafanya kazi  zake ni pamoja na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Ghana.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.