Mchungaji mashimo awataka wananchi kutoingilia maamuzi ya Bunge baada ya kumfuta Ubunge Tindu Lissu.
MCHUNGAJI wa Manabii na Mitume Tanzania, Komando Daud Mashimo, amewaomba wananchi wanaojadili juu ya Bunge kumfuta ubunge aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, waachane na Maneno badala yake waliachie bunge kufanya kazi zake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Leo Kinondoni, amesema ipo minong'ono na lawama zinazoelekezwa kwa Spika wa Bunge juu ya uamuzi huo. Amesema Bunge lina vipengele vyake na Kanuni hivyo tuache kuingilia muhimili huo wenye mamlaka ya Kutunga Sheria hapa nchini.
Amesema Watanzania wengi wamekuwa mbele kuingilia mambo wasiyoyajua kwani kama lipo tatizo kati ya Bunge na Lissu basi Mahakama ipo Sheria zitafuatwa kama Lissu ataona kafanyiwa tofauti na Kanuni za Bunge.
Amesema yeye anafahamu sana kuhusu Lissu kwahiyo sio kila kitu akiseme kwani amekuwa katika maono yake katika utawala wake. Amewataka watu kutomnyooshea Spika wa Bunge mkono kwani sio maamuzi yake ni Sheria na Kanuni za Bunge ndio zilizo mfuta Ubunge.
Hivyo amewaomba Watanzania kuachana na Maneno ambayo yanaweza kuhatarisha hali ya Usalama badala yake wajikite katika kuliombea Taifa ili lipige hatua.
" Nataka niwaambie ndugu zangu hata kama kutatokea watu kukushawishi juu ya maamuzi ya Spika nakuomba achana naye kwani unaweza kuingia katika machafuko yanayoweza kuhatarisha Usalama wa nchi hii mambo ya Bunge tuliachie Bunge kwakuwa sisi hatujui Kanuni wala Sheria za Bunge" Amesema Mchungaji Mashimo.
Pia amewataka Wanasiasa wafanye uchaguzi kwa Amani na utulivu na kutofanya vurugu zitakazo pelekea Taifa kuingia kwenye Machafuko.
Aidha amewatahadharisha vijana kutotumika na wanasiasa katika uchaguzi ili kuepuka mvurugano na kuchafua Amani ya Taifa hili.
Post a Comment