Header Ads

Das Ilala awaasa Watumishi wa Staafu Magereza katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania Ukonga kuwekeza pensheni zao katika Ujasiriamali.






 KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala , Sheila Edward Lukuba, amewaasa Watumishi Wastaafu Jeshi la  Magereza waliostaafu Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Magereza Ukonga kuwekeza katika Biashara na kuwa Wajasiriamali Mara baada ya kupokea Pensheni zao.


Hayo ameyasem leo  akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Mh Sophia Mjema, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Wastaafu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania Ukonga Jijini Dar Es salaam Leo Julai 28/ 2019.

Akizungumza na Wahitimu hao, Katibu Tawala Sheila Edward Lukuba, amesema ni vyema Waastafu hao wajikite katika Ujasiriamali ili Pensheni watakazo zipata ziwe kujizungusha na wazalishe zaidi.




 Amesema kuwa , awali walikuwa wakitegemea sana mshahara sasa mshahara hakuna lazima waweke akiba na kusoma alama za nyakati.



Aidha, amesema kuwa kitendo cha kuhitimisha utumishi salama ni hatua kubwa na muhimu tena  inayo stahili pongezi.


" Hongereni sana Wastaafu, nafahamu fika muda wote  mliodumu katika utumishi mmekabiliana na mambo mengi magumu na mepesi na mlikabiliana nayo kwa hekima, busara na nidhamu, hivyo kuna msemo wa Kiswahili usemao " Ukiona nyani mkongwe, jua amekwepa mikuki mingi" ni wazi kabisa kwenu pia katika utumishi wenu kwa muda wote  huo mmekutana na mengi na mengi mazuri na mabaya, yanayoudhi na yaliyowafurahisha lakini mlipambana nayo na kumilia" Amesema DAS.

 Amesema amefarijika baada ya kusikiliza risala yao huku akisema ni ukweli mtupu kuwa bado jeshi la  Polisi linakabiliwa na changamoto mbali mbali.


Lakini mbali na hayo, amewataka Wastaafu wapatapo Pensheni zao wajitahidi kuwa karibu na familia zao na wake zao.

Pia amesema bado ushauri na mawazo yao yanahitajika sana kutokana bado ni askari na wana mbinu nyingi za kijeshi ambazo zitaweza kusaidia Jeshi kusonga mbele.

Pia amewaomba wakina baba kuachana na michepuko ya nje " nyumba ndogo " badala yake wawashirikishe wake zao katika kuleta Maendeleo katika familia.


 Pia amewasistizia na wakina mama kuachana na Vi Ben Ten kwani huko kuna weza kupelekea kuyumba kwa familia na malezi bora ya watoto.


Pia amewaomba Wastaafu kuhakikisha wanaizungumzia vizuri Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kutekeleza vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Amesema ipo  miradi mbali mbali inayotekelezwa ikiwamo Treni ya umeme, mradi wa umeme Rufiji, Ununuzi wa ndege pamoja na kuongezeka kwa Vituo vya Afya na Hospitali hapa nchini.


 Mbali na hayo amewaomba Wastaafu wasitoe taarifa hovyo  za Jeshi mpaka pale Jeshi litakapo wahitaji kushirikiana nao kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.


Naye , Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Joe Matani, amewataka Wastaafu hao kuendelea kulinda nidhamu, busara na heshima katika Jamii .



pia amempongeza DC Mjema kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia utekelezaji katika Wilaya yake.

 " DC Mjema ni Jembe, tumekuwa Mara kadhaa tukimualika kwenye shughuri zetu amekuwa mwepesi sana kujumuika nasi, ndio maana Leo tukaona tuwe nae lakini ujio wako Katibu Tawala bado tuna muona mama yetu Mh Sophia Mjema yupo nasi"Amesema ACP Joe Matani.


 Mbali na hayo amesema Jeshi hilo  la  Magereza linakabiliwa na changamoto nyingi, miongoni mwa hizo changamoto ni pamoja na Ufinyu wa Bajeti, Uchakavu wa Majengo, Uchache wa Magari, Ujenzi wa nyumba za Watumishi askari, Viwanja pamoja na Utatuzi wa migogoro kati ya Jeshi la Magereza na Raia.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.