Header Ads

DC Mjema aahidi kupanua Ujenzi wa Msikiti na Madrasa ya Munarawara Msasani Kibonde Maji.




MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, ametangaza kupanua ujenzi wa Msikini na Madrasa ya Munarawara Uliopo Msasani Kibonde Maji

Hayo ameyasema Leo mara baada ya kutembelea Madrasa hiyo  Leo Juni 16 mwaka 2019 ikiwa ni mualiko rasmi katika uchangiaji wa ujenzi huo.

Aidha, licha ya changamoto alikutana nazo  kutoka katika Uongozi huo, lakini amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imetenga mikopo ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Hivyo, amewataka wakina mama na Vijana wajipange vizuri katika vikundi vyao kisha atawasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kuona jinsi ya kuweza kuwasaidia.


" Ifike wakati tunaendesha dini lakini tusisahau Uchumi, kwani maisha yetu yana mahitaji mengi sana, lazima changamoto zetu tuzitengenezee mikakati kwa kutafuta ridhiki halali inayopendeza Mwenyezi Mungu" Amesema DC Mjema.

Pia amewaambia yupo  tayari Kuona anafanikisha suala la  ujenzi kwani ameshakuwa katika maongezi na mfadhili mmoja ambapo watafika eneo husika kwa ajili ya Kuona Mazingira pamoja na wanafunzi wa Madrasa.

Hata hivyo DC Mjema , amesema kuwa ili ujenzi uanze miongoni Mwa vitu kama vile kutoa mchoro wa Msikiti pamoja na madrasa katika Kuona ni aina gani ya muonekano kama kutawanyika au kupanda juu ( ghorofa
), kupata mahali ambapo kuna nafasi ili kutoa maeneo ya kutafutia ridhki pamoja na kiwanja

Hata hivyo licha ya changamoto zao, lakini ameweza kutoa kiasi cha Shilingi 200000/=kama pesa ya mahitaji madogo madogo kama vile kununulia umeme nk.
.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.