DC Mjema azungumzia upatikanaji wa mtuhumiwa anayedaiwa kufanya mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Kampala Gongolamboto.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amempongeza Kamishina msaidizi wa Polisi RPC Mkoa wa Ilala kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kupatikana kwa mtuhumiwa wa mauaji ya binti mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa akisoma Chuo cha Kampala kilichopo Gongolamboto.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kumeleta heshima kwa Polisi na kuwafanya Wananchi kuwa na imani na Jeshi la polisi kwamba linafanya kazi.
Amesema baada ya kupatikana kwa mtuhumiwa , amewataka Wananchi waishi kwa amani kwani Serikali ni moja na hakuna serikali nyengine ya uchochoroni itakayowasumbua Wananchi.
Pia ametoa shukrani za dhati kwa RPC Ilala, Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Dar Es salaam Razaro Mambosasa pamoja na Naibu Waziri mambo ya ndani kwa kuhudhuria katika msiba huo.
Amewataka Wananchi waishi kwa Amani, kwani Serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli, ipo macho na inawajali Wananchi wake na inafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na Sheria.
Pia amesema pale ambapo matukio kama hayo yanatokea basi waachiwe Jeshi la Polisi wafanye taratibu zao.
" Nipende kumpongeza Kamanda RPC kwa kupiga kambi ya siku mbili na nusu na sasa tayari mtuhumiwa amepatikana ,hivyo upelelezi utakapo kamilika atafikishwa Mahakamani " Amesema DC Mjema.
Aidha amesema kuwa mtuhumiwa amepatikana na operesheni sio mwisho itaendelea kuhakikisha maeneo ya Gongolamboto , Ukonga yanakuwa salama na Wananchi waweze kufanya kazi zao na kuendeleza Taifa lao.
Naye Kamishina Msaidizi wa Polisi RPC Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembera, amesema mtuhumiwa amepatikana Jana usiku Madale, lakini kwa sababu za kiupelelezi asingeweza kumtaja jina licha ya mtuhumiwa Hugo kukili kuwa amehusika na mauaji hayo.
Aidha amesema timu yake ya upelelezi inaendelea na kazi ya kufuatilia vitu ambavyo ni muhimu katika kuunganisha ushahidi.
Amesema taarifa zaidi Kamishina wa Polisi Kanda maalumu ya Dar Es salaam , Razaro Mambosasa atazitoa katika vyombo vya Habari. Amesema mtuhumiwa aliyekamatwa ndiye atakayesaidia kupata mtandao wa waharifu , Ukonga, Kinyerezi, Chanika na maeneo mbali mbali mkoa wa Dar Es salaam ili kukomesha uharifu.
Post a Comment