Header Ads

RC MAKONDA ATOA UFADHILI WA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 KUTOKA FAMILIA ZISIZOJIWEZA*.g



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo Juni 22 *ametimiza ahadi* ya kutoa *ufadhili wa matibabu ya upasuaji wa moyo* kwa watoto *10* kati ya *60* alioahidi kugharamia matibabu yao *hadi pale watakapopona.*

*RC Makonda* amesema ameamua kutoa ufadhili wa *watoto 10 kila mwezi* kwa kipindi cha *miezi sita* ambapo zoezi la *upasuaji* kwa watoto hao litaanza rasmi siku ya *Jumatatu ya Juni24* kwenye *Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.*

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea *hundi ya Shilingi Milioni 10* kutoka taasisi ya *Patel Samaj* kwaajili ya matibabu ya *watoto 10 kati ya 60* kutoka *mikoa* mbalimbali *RC Makonda* amesema *walengwa ni watoto wanaotoka kwenye familia maskini* ambazo zimepoteza *matumaini* kutokana na *ukubwa wa garama za matibabu* ambapo inaelezwa *gharama ya upasuaji ni kwa mtoto* mmoja ni kati ya Shilingi *Milioni 8 hadi 10.*

Aidha *RC Makonda* ameipongeza *Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete* kwa kazi kubwa na nzuri ya kutoa *huduma za kisasa* kwa wagonjwa jambo lililosaidia *kuokoa gharama zilizokuwa zikitumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi.*

Hata hivyo *RC Makonda* ameishukuru taasisi ya *Patel Samaj* kwa kumuunga mkono kupitia *ufadhili matibabu* kwa watoto hao ambapo ameziasa *taasisi, makampuni na watu binafsi* kusaidia matibabu kwa *wenye uhitaji.*

Kwa upande wao *wazazi wa watoto waliopata ufadhili* huo kutoka mikoa mbalimbali wamemshukuru *RC Makonda* ambapo wameeleza kuwa *kwa muda mrefu wamehangahika kutafuta pesa ya matibabu kwa watoto wao bila mafanikio kutokana na ukubwa wa garama.*

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.