Header Ads

DC Mjema awatahadharisha wafanya Biashara wasio kuwa wasafi katika maeneo yao ya kazi.




MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, ametoa onyo  Kali Leo kwa wale wafanya Biashara wasio kuwa wasafi katika maeneo yao ya kazi.

Kauli hiyo  ya kalipio, ameitoa Leo wakati Wa zoezi la  usafi lililofanyika Wilaya ya Ilala leo  Juni 8/2019, ambapo kiwilaya zoezi hilo la usafi limefanyika Kata ya Mchikichini na Jangwani, ambapo kwa Jangwani ameendesha zoezi la  kunyunyiza dawa za kuua vimelea vya mbu Wa Dengue pamoja na Kipindu pindu.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari, amesema zoezi hilo halitaishia Leo bali litakuwa endelevu kwa kila siku.

Amese kuwa bado kuna Mazingira ya makazi ya watu hayaridhishi hata maeneo ya wafanya Biashara hali ni tete kiusafi, Hivyo ametoa onyo kwa yeyote asiyefanya usafi katika eneo lake la  kazi nyumbani kwake atatozwa faini kubwa ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wasiokuwa wasafi.

Amesema anashangazwa sana Wilaya ya Ilala ipo mjini kwenye miundombinu yote lakini uchafu umekuwa kikwazo na kusababisha magonjwa ya milipuko kama vile kipindu pindu na dengue.

Aidha amesema ameshangazwa sana Kuona kila ugonjwa Wa kipindu pindu unapoingia hapa nchini Wilaya ya Ilala inaongoza jambo ambapo amepanga kulifanyia kazi kwa ufanisi mkubwa kuhakikisha ilala inakuwa salama na safi.

" Ilala tuna takwimu mbaya ya ya Wagonjwa Wa kipindu pindu, awali tulipokea taarifa ya watu 16 waliolazwa kwenye kempu zetu za Wagonjwa Wa mlipuko lakini tulimpoteza mtu  mmoja tu aliyefariki kutoka Kata ya Vingunguti hapo hapo tumepata tena Wagonjwa 9 , hii sio picha nzuri, hakuna roho mbili duniani lazima tuwe wasafi katika makazi yetu na maeneo yetu ya kazi kuzuia hili" Amesema DC Mjema.


Pia ameshangazwa Kuona bado baadhi ya watu wanatumia mifuko ya plastiki, lakini ametoa agizo wale wote  ambapo hawajasarimisha mifuko hiyo  watachukuliwa hatua Kali za kisheria. .

Amewaagiza bibi Afya na Bwana Afya wasikae ofisini badala yake  watoke na kwenda mitaani kuangalia hali za usafi kwenye biashara na maeneo ya watu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.