Header Ads

Kaimu Meya Ilala atoa Vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki 3 kuwasaidia Vijana katika kukuza Michezo.




KAIMU MEYA Ilala atoa jumla ya Shilingi Milioni 1 na laki 3 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri na Jeshi la  Polisi baada ya kuwapatia Kituo cha Polisi Vingunguti  King'amuzi cha Azam.


Akizungumza na waandishi wa Habari, amesema kutoa vifaa hivyo vya Michezo Seti 6 za Jezi ni moja ya kuendeleza Michezo katika kata Hiyo na kutekeleza ilani ya CCM ya kuendeleza Michezo kwa Vijana.

Miongoni Mwa vifaa alivyotoa ni pamoja na Seti 6 za Jezi za mpira wa Miguu na King'amuzi cha Azam kwa Kituo cha polisi Vingunguti.

Amesema King'amuzi hicho kitawasaidia Kuona utendaji na mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt John Magufuli katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Miongoni Mwa timu zilizopewa Jezi hizo Leo Julai 23/2019 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Vingunguti Mtaa wa Mtakuja ni pamoja na timu za mazombi,kijiti cha mishemishe na B13 .baiskeri ya mlemavu na king,amuzi kwa jeshi LA polisi Vingunguti jumla thamani yake vitu 1,3,10000

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.