Header Ads

RC Makonda aridhishwa na Maendeleo ya Mradi wa Nyumba za Askari Magereza Ukonga.





























Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbli ya jijini Dar es Salaam, leo ametembelea mradi wa maghorofa 12 ya askari Magereza unaosimamiwa na Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ)uliopo Ukonga jijini hapa.

Ambapo hapo awali mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Ujenzi nchini TBA na Jeshi la Magereza kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuukabidhi mradi huo kwa JWTZ.

RC Makonda ameonesha kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kumpongeza msimazi wa Oparesheni ya mradi huo Brigedia Charles Mbuge na mainjinia huku akiwa na imani kuwa ndani ya miezi miwili na nusu mradi huo utakuwa tayari.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Oparesheni ya mradi Brigedia Mbuge ameeleza kuwa katika ghorofa ya chini majengo yote 12 yamefikia asilimia 90% bado asilimia 10% kumaliza kujenga tofali na kuongeza kuwa ndani ya mud wa wiki moja watakuwa wamemaliza ghorofa ya pili.

Ujenzi wa mradi huo ukikamilika inakadiriwa kuwa familia 172 zitapata makazi huku maghorofa 8 yakiwa ya askari na manne 4 ya maafisa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.