Header Ads

RC MAKONDA AMTOLEA UVIVU MHANDISI MSHAURI BARA BARA YA KILONGA WIMA MRADI UNAOFADHILIWA NA BENKI YA DUNIA.




MKUU Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam, Mh: Paul Makonda, amemjia juu Mhandisi Wa kipande cha bara  bara kilichopo Kilonga Wima Mara baada ya kukuta thamani ya pesa haiendani na mradi husika. Ameyasema hayo ikiwa ni Siku mbili tangia kuanza kwa ziara yake  ya kukagua miradi ya Maendeleo na kimkakati inayoendelea katika Mkoa Wa Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari Leo, RC Makonda amesema mradi  huo ambao una kilomita 2.1 umetumia fedha kubwa ambazo zingetumika katika bara bara nyingine.

Amesema kuwa  mpaka sasa bara bara hiyo haijakidhi na kuendana na thamani ya pesa kwani inaonekana kutokufikia ubora unaotakiwa.


Aidha amesema kuwa  katika tathimini yake  amegundua kwamba miradi inayoendeshwa na DMDP inatumia gharama kubwa tofauti na miradi ya TANROAD lakini bado miradi ya DMDP inakosa ubora unaozingatia thamani ya pesa inayotolewa.

  Amesema kwamba, ipo  haja ya kurekebisha mifumo ya kisheria inayotumika katika miradi hiyo ili kuweza kupunguza gharama kubwa zinazotumika sasa na zile zinazobakia zitumike katika miradi mungine.

" Mkoa wetu unachangamoto sana za bara bara pamoja na jitihada zote bado kuna  bara bara mbovu sasa tukiokoa pesa hizi kwa matumizi makubwa tutaweza kuokoa milioni 800 ambazo tutazipeleka katika miradi mingine ya bara bara na Jiji letu likawa na miundombinu mizuri ya bara bara zenye viwango " Amesema RC Makonda.

Sambamba na kuwepo kero hiyo ya bara bara , ameshauri DMDP kushirikiana na TARURA ili kuingilia kati pesa za miradi ya bara bara zisitumike kihorera.

Kwa upande wa  Mhandisi Mshauri kutoka mradi wa Benki kuu ya Dunia, Eng: Henrdy  Ngogolo, amesema miradi huo una thamani ya pesa Bilioni 4.5  na utatumika kupitisha uwezo Wa tani 10.

Amesema mpaka sasa mradi  huo umebakia asilimia 46% na washatumia bilioni 1.7.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.