Header Ads

RC Makonda aweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Madarasa , Vyoo na Mabweni ya walemavu Wa Macho.




MKUU wa  Mkoa Wa Dar es salaam, Mh Paul Makonda, ameweka  jiwe la  Msingi kuashiria kuanzisha shule maalumu ya watoto wenye ulemavu Wa macho. Uwekaji huo Wa jiwe la  Msingi umeendana samba mba  na ukaguzi wa  Mabweni ya wanafunzi hao yenye uwezo Wa kuchukua jumla ya Wanafunzi 80 .


Amesema Shule hiyo itakuwa ya kwanza katika Mkoa Wa Dar es salaam ambapo mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi 24 waliowabaini.

Amemtaka Mkurugenzi Wa Temeke Mh Mwakibibi kuhakikisha fursa za awali ziwafikie kwanza watoto waliopo Wilaya hiyo kabla ya kuongeza watoto wengine katika maeneo mengine.

 " Hii ni fursa niwapongeze mmeanza vizuri sana,Mimi niliguswa sana na walemavu lakini nyie mkaonesha nia fanyeni lakini kabla ya kuchukua watoto wengine hakikisheni waliopo Temeke wanapata nafasi kwanza kisha mchukue wengine" Amesema RC Makonda.


Amesema mpango huo utaenda nchi nzima kwani amegundua watoto hao wanauwezo mkubwa.



 Ujenzi huo Wa Mabweni na Shule ya walemavu Wa macho uliopo Kata ya Tuangoma Wilaya ya Temeke ni wakwanza katika Mkoa Wa Dar es salaam.



 Aidha kwa upande Wa Mkurugenzi Wa Wilaya ya Temeke Lusubilo Mwakabibi, amesema huu ni mwanzo kwani wapo katika mpango Wa kuhakikisha wanajenga shule tano  ili kuwasaidia walemavu hao na Kuona nao wanapata haki sawa ya elimu kama ilivyo kwa watu wengine.


Amewataka Wazazi wasiwafiche watoto zao wajitokeze kwa wingi ili watoto hao wapate elimu.


" Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli, ameleta elimu bure hivyo hapana budi ndugu zetu wenye ulemavu Wa macho wapate haki hiyo kikamilifu kuelekea uchumi wa  kati" Amesema Mwakabibi.


 Katika hitimosho RC Makonda amesema kubwa alilogundua ni kwamba Viongozi wameonesha ubunufu Wa kutatua kero za wananchi hususani katika miradi ya bara bara Temeke wamejitahidi sana kwani wameweza kuokoa pesa nyingi za bara bara tofauti na Wilaya ya Kinondoni.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.