Header Ads

RC MAKONDA AZIDI KUFICHUA MADUDU MIRADI YA DMDP, AWATAKA TAKUKURU KUANZA UCHUNGUZI MARA MOJA*.






Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amemuagiza Mkurugenzi wa *TAKUKURU* Mkoa huo kufanya *uchunguzi wa utaratibu wa upatikanaji wa tenda kwenye miradi ya DMDP* baada ya kubaini *matumizi mabaya ya fedha za serikali* katika miradi hiyo.

*RC Makonda* amesema haiwezekani kuona *Kilomita Moja* ya Barabara ya DMDP *Wilaya ya Kinondoni* inajengwa kwa Shilingi *Billion 2.7* wakati kwa *Wilaya ya Temeke* barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi *Milioni 900.*  

*Mhe. Makonda* amebaini *madudu* hayo wakati wa mwendelezo wa *ziara* yake ya ukaguzi wa *miradi ya maendeleo* kupitia fedha zinazotoka *Serikali Kuu, Halmashau na pesa za wahisani* ambapo amekwazwa na matumizi mabaya ya *fedha za mkopo* kutoka *Bank ya dunia.*

Aidha *RC Makonda* amesema kuwa Barabara  za *DMDP* zimekuwa zikijengwa kwa *kiasi kikubwa cha pesa* kuliko zile za *TANROAD* ambazo kwanza zina ubora mkubwa, *uwezo wa kubeba mzigo mkubwa* na pia ni Pana.

Katika ziara hiyo *RC Makonda* ametembelea miradi ya Ujenzi wa Barabara,Hospital na Shule ambapo *ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo* na kuwataka kuongeza *kasi.*

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.