Header Ads

RC Makonda awataka Wananchi kutochagua Viongozi uchwara wasio na uwezo Wa kutatua kero zao














Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda awataka wananchi kuwachagua viongozi wenye uwezo wa kuwatatulia kero na changamoto zinazowakabili.

Makonda ameyasema hayo Leo alipokuwa Katika mwendelezo wa  Ziara yake ambapo alikuwa Katika Wilaya ya Ubungo ambapo amepata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Mbezi Makabe.

"Tusifanye kosa la kuchagua watu kwa sababu wanauwezo wa kuongea sana au wenye uwezo wa kusema,tuchague watu wenye uwezo wa kuchukua kero zetu na wana sehemu za kuzipeleka na kuzitafutia  ufumbuzi" Amesema Makonda.

Aidha amehaidi kujenga kituo Cha afya Pamoja na hospitali ya Wilaya ambapo Amesema atazungumza na Waziri wa Tamisemi Mhe. Suleiman Jaffo aweze kusimamia hayo na kuweza kuwaletea wananchi hao Maendeleo.

Aidha ameshangazwa na mwenendo wa baadhi ya viongozi kushindwa kutafuta eneo la kuongeza madarasa mawili na kubaki kusema wamerithi eneo ambalo halitoshi kujenga madarasa hayo.

Katika hatua nyingine ametembelea Ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo itakuwa na ofisi ya mbunge ndani yake hivyo ametoa maelekezo kuwa ofisi ya mbunge wa Jimbo la ubungo ijingwe maeneo hayo ili aweze kuwafikia wananchi wa Jimbo lake.

"Kwenye Ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kuna ofisi mbili za mbunge wa kibamba na mbunge wa Ubungo, nimemuelekeza Mkuu wa Wilaya ahakikishe mbunge wa Ubungo anatafuta eneo la kujenga ofisi Katika Jimbo lake" Amesema Makonda.

Katika Ziara hiyo RC MAKONDA ametembelea miradi ya maji ambapo Ujenzi wa kisima Cha maji Mbezi Makabe, Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya  Ubungo,Ujenzi wa kituo Cha mabasi Mbezi Luis Pamoja na Ujenzi wa kituo Cha afya kiamara.

Hata hivyo wananchi wa Mbezi Makabe wamemshukuru Mh.Makonda kwenda kuwasikiliza na kuwatatulia migogoro yao ambapo wamesema wanaimani kuwa changamoto zao zitakwisha.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.