Header Ads

Ukosefu wa nidhamu kwa baadhi Viongozi Ubungo ni kikwazo cha Maendeleo: RC makonda.


i



MKUU Wa Mkoa Wa Dar es salaam, Mh Paul Makonda amesema kukosekana kwa nidhamu kwa baadhi ya Viongozi Wilaya ya Ubungo ndio chanzo cha kuzorota kwa Maendeleo. Hayo ameyasema Leo wakati Wa mwendelezo Wa ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo iliyopo katika Mkoa wake.


Akizungumza na waandishi Wa Habari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Ubungo, RC Makonda, amesema wapo baadhi ya Viongozi wanaoshindwa kutoa neno la  asante kwa Viongozi wao  wakubwa kipindi wanapokabidhiwa miradi ya Maendeleo huku wakijikuta mabingwa Wa kutoa Maneno Makalu juu ya miradi hiyo bila ya kukumbuka shukrani kwa yule aliyewapatia.


Amesema kitendo cha Meya Wa Ubungo , Mh Boniface Jacob, cha kutotoa neno la  shukrani huku akitanua kifua na kuaminisha Wananchi kwamba miradi hiyo wao  Manispaa ndio wameidhinisha na yeye alitia saini ni kukosa hekima na badala yake alitakiwa kwanza kutoa neno la  shukrani kwa Mh Rais Dkt John Magufuli.




Pia amesema Wananchi watambue kwamba hakuna Nguvu ya Manispaa hata moja mkoa Wa Dar es salaam iliweza kupata fedha za miradi bila Nguvu ya Rais ambaye fedha zote zilitengwa kwa maelekezo kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi. Amewataka Wananchi kuwachagua Viongozi wachapa kazi na wenye uwezo Wa kutatua kero zao badala ya kuchagua wapigaji domo na wapinzani Wa Maendeleo.




" Kuna baadhi ya Viongozi wenu wanawanyima sana Maendeleo, hapa nilitegemea Meya wenu atampongeza Rais wetu Dkt John Magufuli kwa kufikiria mambo makubwa kuleta miradi ya Maendeleo kwa Wananchi yeye amekuwa akijitamba kwamba ametia saini huu ni upumbavu unafikiri saini zinasaidia nini bila ya Mh Rais kufikisha pesa hizo za miradi?  Ukiangalia miradi mingi  niliyoifanya ni Nguvu ya Rais sasa hata pongezi hatoi baraka  ya kuwalisha Maneno Maneno ambayo hayana busara miradi" Amesema RC Makonda.

Pia amesema Wananchi watambue kwamba hakuna Nguvu ya Manispaa hata moja mkoa Wa Dar es salaam iliweza kupata fedha za miradi bila Nguvu ya Rais ambaye fedha zote zilitengwa kwa maelekezo kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi.

 Amewataka Wananchi kuwachagua Viongozi wachapa kazi na wenye uwezo Wa kutatua kero zao badala ya kuchagua wapigaji domo na wapinzani Wa Maendeleo.

Amesema katika mpango Wa Ofisi za Walimu Meya , Boniface Jacobo, aliupinga mpango hyo ndio maana mpaka sasa hakuna kinachofanyika tofauti na wilaya nyingine ambazo mpaka sasa zina Ofisi za waalimu na nyingine zinatengenezwa ili waalimu waishi katika Mazingira rafiki na kuongeza kiwango cha ufaulu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.