Header Ads

RC Makonda awafuta machozi Wajane kupata haki zao za Mirathi.






  MKUU wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mh Paul Makonda, leo  amewafuta machozi Wajane kwa kuwakutanisha na Wanasheria kupata haki zao za mirathi jambo ambalo limekuwa ni changamoto kwao.


  Kongamano hilo la  kuwakutanisha Wajane , limefanyika lei kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini  Dar Es Salaam.

  Aidha RC Makonda, amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili Wajane ni pamoja na suala la  ardhi  na kukosa haki zao baada ya kuondokewa na wanaume zao.

  Amesema ili kuzuia hayo, amewataka Wanaume wabadilike ili kuzuia mifumo ya kufikiri katika familia zao ili watakapo tangulia mbele za haki familia zao ziishi vizuri.  

RC Makonda amesema lengo la  kongamano hilo ni pamoja na luwatia Moyo Wajane, kuangalia mifumo ya kusheria kama unafanya kazi ipasavyo.

  Amesema kuwa moja ya mambo aliyotaka kuyafahamu ni pamoja na kujua ni namna gani ya urithi ulioachwa unatumika ipasavyo na namna ya kupata mikopo ya 4% kwa wakina mama pamoja na tabia za malezi kwa wakina mama kabla na baada ya mume kufariki.

 Amesema Mwanaume yeyote makini ni yule anayewaza ni namna gani akitangulia mbele za haki familia yake  itakavyoishi .

 Pia amesema mambo ya kisheria yana ukakasi hivyo lazima wanasheria lazima waeleze haki za marehemu kwa familia zao.

  " Hapa nimegundua kitu sijafanya kongamano hili ili nipate sifa bali  nimeguswa na matatizo yanayowakumba Wajane baada ya watu 300 kufika Ofisini kwangu, hivyo kwa uwezo wa Mungu tunaimani haki za Wajane zinakwenda kupatikana Mara moja" Amesema RC Makonda.  

Amesema Rais John Magufuli anachukizwa sana Kuona Wajane hawapati haki zao kwa wakati .

 Amesema anachokifanya yeye ni kukusanya taarifa za kesi za Mirathi na kumpelekea Waziri wa Sheria ili hatua zichukuliwe wapate haki zao ndani ya miezi 3 ijayo.  

Amewataka Wazazi wasiwaache watoto kuiga tabia mbovu na amesema kuondoka kwa baba Wazazi wasikubali watoto wakatumbukia katika dimbwi la  shetani.

  Hata hivyo amewataka Wazazi wasiwakatie tamaa watoto walio walea  miezi 9.

 Pia amewasihi Wajane pamoja na kupata haki zao na mafundisho wahakikishe Mungu anawatawala katika maisha yao.    Amesema kuna haja ya madeni ya wa marehemu kuwekewa bima ili familia zao ziweze kunufaika na Mali zao.

    Pia kujua ni muda gani wa kisheria uliowekwa kwa Mama mjane  ili kesi yake  inamalizika na wanapata majibu .  

   Amesema ataanda utaratibu wa kukutana na asasi za kisheria kujifungia ili kupitia malalamiko yote na kuyapatia majibu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.