RC Makonda afurahishwa na kasi ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilala iliyoko Kivule
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,amempongeza Kasi ya Ujenzi wa hospitali ya Kivule iliyopo Katika Wilaya ya Ilala.
RC Makonda amefikia hatua hiyo Mara baada ya kufanya Ziara Katika Wilaya hiyo na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ambapo amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa kivule, Ujenzi wa Soko la kisasa kisutu, Hospitali ya Buguruni, Barabara ya Kiwalani Pamoja na Barabara ya Gerezani ambayo ni miradi mkakati.
Amesema mradi wa Ujenzi wa hospitali ya Wilaya inategemewa kukamilika mwezi June mwaka huu ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kukahakikisha anaendelea kuusimamia vyema.
" Kwanza kabisaa nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kusimamia vyema ujenzi wa hospitali hi ya Kivule Kasi wanayoenda nayo Ni nzuri na matumaini yangu Hadi kufikia June 30, mwaka huu utakuwa umeisha" Amesema Makonda.
Ameongeza kuwa miradi yote hiyo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa lengo la kuwasaidia wanyonge ambao Ni wananchi wa hali ya chini.
Amesisitiza kwamba Rais John Magufuli anataka kuona huduma zinamfuata mwananchi na siyo mwananchi anaifuata huduma na kuongeza kwamba hospitali hiyo itatumika kwa wananchi wote ambao walikuwa wakienda kufuata huduma katika Hospitali ya Amana ambao wanaoshi maeneo hayo.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema watu waache dhana kwamba Kuna watu wanaotumia wanyonge kwa manufaa yao binafsi kwani Katika Serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kuwainua na kuwatetea wananchi wanyonge.
Post a Comment