RC MAKONDA AMTAKA DC ILALA KUENDELEZA UKALI USIMAMIZI WA MIRADI YA UTATUZI WA KERO SUGU ZA WANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amemuhimiza Mkuu wa Wilaya Ilala kuendeleza *ukali* katika usimamizi wa *Miradi ya Maendeleo* inayolenga kumaliza *kero sugu* zilizokuwa *mwiba* kwa wananchi ilikuenda sambamba na *utekelezaji* wa ahadi ya *Rais Dkt. John Magufuli* aliyoitoa wakati wa uchaguzi.
*RC Makonda* ametoa kauli hiyo wakati wa *mwendelezo wa ziara* yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambaoo akiwa kwenye ukaguzi wa *ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ilala* inayogharimu zaidi ya *Bilioni 1.5* RC Makonda ameagiza *ujenzi huo kukamilika na kukabidhiwa kabla ya Juni 30* mwaka huu.
Aidha *RC Makonda* amesema uwepo wa hospital hiyo katika eneo la *Kivule* itasaidia wananchi wa ukanda wa *Pugu, Majoe,Chanika,Gongolamboto* na maeneo mengine kupata *huduma za afya* jirani na maeneo wanayoishi.
Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema *serikali ya awamu ya tano* imedhamiria kuhakikisha *inawasogezea wananchi huduma zote muhimu* ikiwemo *Maji, Barabara, Afya,Elimu, Masoko* na kuhakikisha *wanyonge* wanapata huduma bora na haki sawa.
Hata hivyo *RC Makonda* amesema kwenye mkoa wa Dar es salaam tuna *miradi ya maendeleo* yenye thamani ya zaidi ya Shilingi *Trillion 3* hivyo ameagiza *wazawa* kuchangamkia fursa ya ajira zinazopatikana.
Katika hatua nyingine *RC Makonda amesema serikali imedhamiria kutoa ya elimu ya ufundi bure kwa vijana wanaofanya kazi ya ufundi na baada ya mafunzo watapatiwa vyeti vya kuwawezesha kutambulika.*
Post a Comment