Mchungaji Komandoo Mashimo azuia kimbunga Mtwara.
MCHUNGAJI Wa Mitume na Manabii Tanzania, Daud Komandoo Mashimo, amefanya maombi ya Nguvu katika kuhakikisha kimbunga ambacho kilibashiriwa kwenye mkoa Wa Mtwara na maeneo mengine.
Mchungaji huyo amesema lengo la kufanya maombi hayo ni kuzuia athari zitakazo wakumba Wananchi ikiwamo kupoteza maisha na Mali zao.
Amesema maombi yake yalitokana na roho ya kiimani ya kutaka kuliombea Taifa na Maeneo yaliyobashiriwa ikiwamo Mkoa Wa Mtwara.
Amesema maombi hayo yalilenga kupata baraka kwa Mwenyezi Mungu ili Wananchi wasipate madhara.
Amesema Rais Dkt John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuijenga Tanzania hivyo neno la Mwenyezi Mungu ndilo pekee lililoponya kimbunga hicho na kufanya maeneo tabiriwa kuwa salama.
" Hawa ni Wananchi wenzetu maombi haya niliyafanya kwa njia njema kabisa kwa Wananchi waliokuwa na hofu na mashaka katika maisha yao hivyo Mwenyezi Mungu alitenda miujiza na kimbunga kikashindikana" Amesema Mchungaji Mashimo.
Amesema madhara ambayo yangetokana na kimbunga yangekuwa makubwa na kusababisha kupoteza Nguvu katika hususani katika ujenzi Wa Taifa kuelekea uchumi Wa Kati.
Amesema bado atazidi kuliombea Taifa pale ambapo jambo litabashiriwa au katika maono yake.
Amesema Kimbunga hicho alikiombea kiende baharini nasio kufikia katika makazi ya watu.
Post a Comment