ABOOD AITAKA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI KUWA NA MAONO YA MAENDELEO NA KIUCHUMI.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe.Dkt. Abdulaaziz Abood, ameshauri na kuelekeza Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini kuhakikisha inakuwa na maono ya maendeleo na Kiuchumi kwa Kuanzisha Miradi Mbalimbali.
Hayo ameyasema Februari 27/2024 Kwenye Kikao cha Baraza la Wazazi CCM la mwaka katika ukumbi wa CCM Kata ya Kingo.
Mhe. Abood, amesema haiwezekani Jumuiya kuwa
ombaomba wakati wanaweza kubuni na kuweka mikakati ya kuanzisha vitega uchumi ambavyo
vinaweza kuwa chachu ya kujikwamua kiuchumi.
“Kwa kweli haiwezekani Jumuiya Kubwa Kama Wazazi kuwa
ombaomba wakati tunaweza kufanya mambo yakatusaidia kiunuka kiuchumi, nimeona
kilio cha Bwawa la samaki niwaambieni mradi huu utakamilika na samaki mtakula,
niwatoe hofu viongozi laleni usingizi mzuri mimi Mbunge wenu nipo nawakabidhi
shilingi 1200, 000/= Kama sehemu ya kianzio cha mradi wenu na siku nikitembelea
kwenye Mradi nitaona nikitu gani cha Kujazia" Amesema Mhe. Abood.
Aidha, ameitaka Jumuiya hiyo Kudumisha umoja na mshikamano
ambapo ndio mafanikio makubwa Katika jambo lolote lakini pia mshikamano
utawasababishia kuimarisha na kusimama kidete ili uchaguzi 2024/2025
kuhakikisha wanachukua viti vyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Udiwani.
Aidha, amesema wakiwa na umoja ndio itawapa Dira ya
Kuelekea 2025 Kuhakikisha kura zote za Wilaya ya Morogoro Mjini
zinakwenda kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni msikivu na mpenda watu.
“Kwa Wilaya yetu, Rais amekuwa akitupendelea mno, kila changamoto ya Morogoro
akiipata huitatua mara moja, ukiangalia katika sekta ya Afya, Elimu, Mundombinu
pamoja na sekta ya Maji Mama ametufanyia makubwa sana, kumlipa kwetu ni kwenda
kumpa kura za kishindo ifikapo mwaka 2025 lakini kuchukua viti vyote vya
Uwenyekiti wa Mitaa Uchaguzi wa mwaka 2024 hadi ngazi ya Udiwani Mwaka
2025" Ameongeza Mhe. Abood.
Hata
hivyo, amewakumbusha Viongozi wa Jumuiya ya wazazi kwamba bado wana
jukumu kubwa la kutoa elimu, kusimamia malezi bora ya watoto na kuhakikisha
kwamba mazingira ya mitaa yanaimarika ipasavyo ili kuwa na Jamii yenye ustawi
na umakini mkubwa.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM
Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, amesema Jumuiya hiyo ipo
tayari kuonyesha nguvu yake kwa kutoa mchango wake mkubwa kwenda kushirikiana na
viongozi mbalimbali na Wananchi kuhakikisha 2024 wanachukua Viti vyote katika
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Nikuhakikishie Mbunge Wetu wa Morogoro Mjini, sisi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya
Morogoro Mjini tutakuwa mstari wa mbele kupigana usiku na mchana muwa tayari
kukitumikia Chama na kuonyesha mchango Wetu kuhakikisha kinapiga hatua kubwa za
kimaendeleo lakini pia kuhakikisha chaguzi Zote tunashinda kwa kishindo tukianza
na chaguzi Ya wenyeviti wa mitaa ya mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025"
Amesema Kipira.
Aidha, Kipira, amewataka Wajumbe wa Mkutano huo katika ngazi zao za Kata
wahakikishe mabaraza yanafanyika kikatiba,wanaelimisha pamoja na mabaraza
ya Matawi.
Hata Hivyo, Kipira ameyataka mabaraza ya Kata wahakikishe pia wanaunda
Kamati ndogo za Mazingira Elimu na Uchumi ili waweze kuwasaidia kuhakikisha
Jumuiya ya Wazazi inakuwa imara na inakuwa na Mchango Mkubwa kwenye Chama
Cha Mapinduzi.
Post a Comment