Header Ads

BARAZA LA KAZI MANISPAA YA MOROGORO LAFANYA MKUTANO MAALUM KUPITIA MAPITIO YA MPANGO NA BAJETI ZA FEDHA ZA MANISPAA


KAIMU Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Manispaa ya Morogoro, Jeremia Lubereje, ameongoza kikao Maalum cha Baraza la Wafanyakazi la Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la  mapitio ya  mpango na bajeti  ya mwaka wa fedha 2022/2023c, 2023/2024  na mpango wa bajeti ya mwaka 2024/2025.

Katika kikao hicho, kilichofanyika Februari 08/2024 Ukumbi wa Ofisi Kuu ya Manispaa, Mwenyekiti amewapitisha  wajumbe wa Baraza hilo kwenye mpango wa bajeti zote tatu huku akiwahimiza  watumishi wote kufanya kazi kwa bidii ili kukidhi matarajio yaliyokusudiwa.

Wajumbe wa Baraza hilo pia walitoka na maazimio kadhaa ambayo mwenyekiti amesema yale mapendekezo ambayo wameyatoa wajumbe watayazingatia  ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa viwango  vya hali ya juu.

Mwisho, Mwenyekiti wa Kikao hicho, Lubereje, amewataka  watumishi wote wafanye  kazi kwa kujituma, ushirikiano na weledi ili kufanikisha azima yao ya kutoa haki kwa wakati kwa wananchi.

Miongoni mwa agenda nyengine zilizojadiliwa ni miradi ya fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu, miradi ya fedha za mapato ya ndani, miradi ya fedha za Serikali Kuu.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.