Header Ads

ABOOD AITAKA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI KUWA NA MAONO YA MAENDELEO NA KIUCHUMI.



MBUNGE  wa Jimbo la Morogoro Mjini,     Mhe.Dkt. Abdulaaziz Abood, ameshauri na Kuelekeza Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Kuhakikisha inakuwa na maono ya maendeleo na Kiuchumi Kwa Kuanzisha Miradi Mbalimbali.

 

Hayo ameyasema Februari 27/2024 Kwenye Kikao cha Baraza la Wazazi Ccm la Mwaka Katika Ukumbi Wa CCM  Kata ya Kingo.

 

Mhe. Abood, amesema  haiwezekani Jumuiya kuwa ombaomba wakati wanaweza kubuni na kuweka mikakati ya kuanzisha vitega uchumi Ambavyo vinaweza Kuwa chachu ya kujikwamua kiuchumi.

 

“Kwa Kweli haiwezekani Jumuiya Kubwa Kama Wazazi Kuwa ombaomba wakati tunaweza kufanya Mambo yakatusaidia Kiunuka Kiuchumi, nimeona kilio cha Bwawa la Samaki niwaambieni mradi huu utakamilika na Samaki Mtakula, niwatoe hofu viongozi laleni usingizi mzuri mimi Mbunge wenu nipo nawakabidhi shilingi 1200, 000/= Kama sehemu Ya kianzio Cha Mradi Wenu na siku nikitembelea kwenye Mradi nitaona nikitu gani cha Kujazia" Amesema Mhe. Abood.

 

Aidha, ameitaka Jumuiya hiyo Kudumisha Umoja na Mshikamano ambapo ndio mafanikio makubwa Katika jambo lolote lakini pia Mshikamano utawasababishia kuimarisha na  kusimama kidete ili uchaguzi 2024/2025 kuhakikisha wanachukua viti vyote kuanzia ngazi ya chini mpaka udiwani.

 

Aidha, amesema wakiwa na umoja ndio itawapa  Dira ya Kuelekea 2025 Kuhakikisha Kura Zote Za Wilaya Ya Morogoro Mjini  Zinakwenda Kwa Rais Dkt Samia Suluhu Ambaye Ni Msikivu Mpenda Watu.


“Kwa Wilaya Yetu, Rais Amekuwa Akitupendelea mno, kila Changamoto Ya Morogoro akiipata huitatua mara moja, ukiangalia katika Sekta Ya Afya, Elimu, Mundombinu Pamoja Na Sekta Ya Maji Mama ametufanyia Makubwa Sana, kumlipa kwetu ni Kwenda Kumpa Kura Za Kishindo Ifikapo Mwaka 2025 Lakini Kuchkua Viti Vyote Vya Uwenyekiti Wa Mitaa Uchaguzi Wa Mwaka 2024  Hadi Ngazi Ya Udiwani Mwaka 2025" Ameongeza Mhe. Abood.


Hata Hivyo, amewakumbusha  Viongozi Wa Jumuiya ya Wazazi kwamba Bado Wana Jukumu Kubwa la Kutoa Elimu, Kusimamia Malezi Bora ya Watoto na Kuhakikisha Kwamba Mazingira ya Mitaa yanaimarika ipasavyo ili kuwa na Jamii yenye ustawi na umakini Mkubwa.


Naye  Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Wazazi Ya Ccm Wilaya Ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, amesema  Jumuiya Hiyo Ipo Tayari Kuonyesha Nguvu Yake Kwa Kutoa Mchango Wake Mkubwa Kwenda Kushirikiana Na Viongozi Mbalimbali Na Wananchi Kuhakikisha 2024 Wanachukua Viti Vyote Katika Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa.


“Nikuhakikishie Mbunge Wetu Wa Morogoro Mjini, Sisi Jumuiya Ya Wazazi Wilaya Ya Morogoro Mjini Tutakuwa Mstari Wa Mbele Kupigana Usiku Na Mchana Kuwa Tayari Kukitumikia Chama Na Kuonyesha Mchango Wetu Kuhakikisha Kinapiga Hatua Kubwa Za Kimaendeleo Lakini Pia Kuhakikisha Chaguzi Zote Tunashinda Kwa Kishindo Tukianza Na Chaguzi Ya Wenyeviti Wa Mitaa Ya Mwaka 2024 Na Uchaguzi Mkuu Wa 2025" Amesema Kipira.


Aidha, Kipira, Amewataka  Wajumbe Wa Mkutano Huo Katika Ngazi Zao Za Kata A Wahakikishe  Mabaraza Yanafanyika Kikatiba,Wanaelimisha Pamoja Na Mabaraza Ya Matawi.


Hata Hivyo, Kipira Ameyataka Mabaraza Ya Kata  Wahakikishe Pia Wanaunda Kamati Ndogo Za Mazingira Elimu Na Uchumi Ili Waweze Kuwasaidia Kuhakikisha Jumuiya Ya Wazazi Inakuwa Imara Na Inakuwa Na  Mchango Mkubwa Kwenye Chama Cha Mapinduzi.

  


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.