Header Ads

DIWANI BUTABILE AGEUKA MBOGO SUALA LA CHAKULA SHULENI, ATOA MSISITIZO MKALI KWA WAZAZI.

 


DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, Mhe. Thomas Butabile, amewataka Wazazi kuchangia chakula shuleni ili kuendelea kunyanyua Viwango vya ufaulu.

Hayo ameyasema Februari 03/2024 katika Kikao Cha Wazazi wa Kidato Cha Kwanza na Cha Tatu Shule ya Sekondari Mafiga.

Akizungumza na Wazazi walihudhuria katika kikao hicho, amesema maamuzi ya BMK ni kila Shule zilizopo Kata ya Mafiga kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula shuleni.

" Suala la Chakula, hakuna Mzazi atakae pona, makubaliano yetu ni Watoto wale Shule, hicho ambacho Mzazi unachangia ni bajeti ambayo Mtoto angekuwa nyumbani angeitumia tena ingezidi zaidi ya hapo, Waalimu na Bodi ya Shule tusimame kidete kuhakikisha hili linafanikiwa, Watoto wakila wanakuwa na utulivu wa akili na kuendelea kufanya vizuri Shule zetu za mafiga" Amesema Mhe. Butabile.

Mbali na chakula, amesema wanafunzi Watoro Mafiga hawatakiwi hivyo amemuagiza Mkuu wa Shule kuhakikisha wale Watoro ambao ndani ya Siku 3 hawapo Shuleni wafukuzwe na kupewa barua za wito za Wazazi.

Kuhusu Mtaala mpya wa elimu ya Kilimo , Mhe. Butabile amewataka Wazazi kuuelewesha Watoto wao vizuri ili Watoto watumie fursa ya kusoma Mtaala huo ambao unalengo la kuwakomboa Watoto kuwa na ujuzi mara wanapo hitimu elimu zao.


Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Mafiga, Mwl . Robert Marwa, amesema yale yote ambayo Wazazi wameyachangia watakwenda kuyafanyia kazi ili kuendelea kupata matokeo makubwa zaidi ya ufaulu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Grace Kihombo , amewashukuru Wazazi Kwa kuonesha ushirikiano licha ya baadhi ya Wazazi wengine wakionekana kutoonesha ushirikiano kwa kuto kuhudhuria kwenye vikao halali vya kisheria vya Shule.

Katika kikao hicho, Wazazi walikubaliana kuwe na michango midogomidogo ambayo itakuwa ikitumika kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kujipima kwa Watoto wao ili kubaini mapungufu na kuongeza Kasi ya ufundishaji ili Watoto wapate matokeo makubwa zaidi ya ufaulu Kama ilivyo Sasa.

Shule za Mafiga ikiwemo Sekondari na Shule za Msingi ni miongoni mwa Shule zinazofanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa Manispaa ya  Morogoro na Mkoa kwa ujumla.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.