BMK MAFIGA YAKABIDHI MISAADA KWA WAHANGA WA MAJANGA YA MOTO MTAA WA MODOKSI MISUFINI.
WIMBI la kutokea kwa majanga ya moto bado limeonekana bado kuwa ni tatizo sugu kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuweza kuzuia majanga ya moto pindi yananapojitokeza pamoja na kutokuwa na vifaa vya kuzimia.
Hayo yamebainishwa Februari 07/2024 na Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Maendeleo la Kata (BMK) katika kikao cha dharura cha kukabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa Kaya zilizo athirika na majanga ya Moto Mtaa wa Modoksi Misufini.
Butabile, amebainisha kuwa wamebaini kuna baaadhi ya wananchi pindi wanapokumbwa na ajali ya moto wanajikuta wanashindwa kuuzima na kuuzuia usiendelee kusambaa katika maeneo mengine kutokana kutokuwa na vifaa, kuwa na uelewa mdogo juu ya uzimaji wa moto pamoja na kuchelewa kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
Aidha, Mhe. Butabile, amepongeza wadau wote waliochangia wahanga hao ikiwemo Uongozi wa Shule ya Sekondari Mafiga kuchangia 167,450/= kwa kushirikisha wanafunzi na stafu ya waalimu kutokana na kuguswa kwa tukio hilo.
“Kwa sasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na uelewa juu ya kupambana na majanga ya moto pindi yanapotokea, tunakuja na utaratibu wa kuhakikisha tunawafundisha wananchi ili waweze kujifunza jinsi ya kuzuaia moto kwani wakati mwingine wanachelewa kutoa taarifa kutokana na kuamua kuuzima wenyewe na unaposambaa ndipo wanatoa taarifa,”Amesema Butabile.
Kwa upande wake , Katibu wa CCM Kata ya Mafiga, Farida Rajabu, amesema kwamba kutokana na wananchi hao kupatwa na matatizo wamerudishwa nyuma kimaendeleo na kuongeza kwamba Ofisi ya CCM Kata kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maendeleo wataendelea kushirikiana kwa hali na mali kuwasaidai wananachi wake pindi wanapopata matatizo.
Mtendaji wa Kata ya Mafiga, Bi. Amina Said, amesema moto huo ulizuka tarehe 4/2/2024 ambapo chanzo chake ni mlipuko wa gesi ambayo ilisambaa na kuunguza nyumba huku majanga hayo yakipelekea Kaya 12 kuathirika huku kaya 7 zikikosa makazi ya kuishi na kuhifadhiwa Ofisi ya Kata.
Amina ,amesema miongoni mwa misaada hiyo ni nguo, unga, sare za wanafunzi , sabuni , madaftari na mahitaji mengine ambapo Kaya 7 kwa kila kaya 1 italipiwa kodi ya miezi 3 yenye thamani ya shiliingi 30,000/= kwa chumba pamoja na kupatiwa mahitaji hayo na unga Kg 25 kila Kaya kama kianzio cha maisha.
Naye miongoni mwa wahanga hao wa moto,ambaye jina lake limehifadhiwa, kwa niaba ya wahabga wenzake, amesema kwamba kwa sasa wamejikuta katika wakati mgumu sana kutokana na vitu vyote kuteketea kwa moto huo.
“Tunapitia kipindi kigumu, lakini tunashukuru sana Uongozi wa Kata chini ya Mhe. Diwani na BMK yake na Uongozi wa Chama CCM Kata pamoja na wadau wa maendeleo kwa moyo wao wa dhati kwa kutuchangia fedha na vitu mbalimbali kama vile vyakula na nguo na kutupatia sehemu ya kujihifadhi hapa Kata , tumefarijika sana " Amesema Mhanga huyo.
Post a Comment