ADRA TANZANIA ILIVYOJIPANGA KUWA MTETEZI WA HAKI NA MASUALA JUMUISHI YA WATU WENYE UALBINO
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Adra Tanzania,( Adventist Development and Relief Agency (ADRA) limekuwa ni miongoni mwa mashirika ambayo ni mkombozi kwa watu wenye ualbino nchini.
Kwa kuthibitisha hilo, hivi karibuni ,ADRA Tanzania wamekuwa wakiendesha shughuli zao Mkoa wa Morogoro kwa kuwa na programu mbalimbali ambazo zote zimekuwa zikilenga masuala jumuishi kwa watu wenye ualbino.
Katika Mradi wa Afrika ambao unatetea haki na masuala jumuishi kwa Kaya za watu wenye ualbino, mradi huu umegawanyiika katika sehemu kuu 4.
Mongoni mwa sehemu hizo ambazo zipo ndani ya mradi huo ni kuwapatia bima za afya wakina mama wanaoishi na watoto wenye ualbino pamoja na watoto wao, mradi ambao umekuwa na manufaa makubwa sana kwa watu wenye ualbino hususani katika suala zima la huduma za afya kupitia bima ya CHF iliyoboreshwa.
Sehemu nyengine ya mradi huo ni kuanzisha vilabu jumuishi vya watu wenye ualbino mashuleni ambapo katika vilabu hivyo wameshirikisha hata wale ambao sio watoto wenye ualbino ili kuwajengea uwelewa wa pamoja na kuona watu wenye ualbino wana kuwa na haki sawa kama wengine na kupewa haki zote ambazo wanafunzi wanatakiwa kuzipata.
Adra ,wameenda mbali zaidi kwa kuwa na mpango mkakati ambao ni sehemu ya mradi wa afrika wenye utetezi wa haki na masuala jumuishi kwa kaya za watu wenye ualbino ( Action for Right and Inclusion of Children with albinism) kwa kuja na mpango wa mafunzo kwa wakina mama wenye ualbino na kuweza kuwapatia fursa wezeshi ya mitaji mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.
Huu ni mpango ambao utawainua zaidi wakina mama wenye ualbino kuweza kushiriki katika uzalishaji mali na kujipatia mahitaji ya kujikimu kwani watakuwa na mafunzo ya kutosha juu ya miradi mbalimbali na fedha ambazo watawezeshwa zitawasiaida sana kujiingizia vipato kupitia miradi hiyo ambayo watafundishwa.
Mwisho, Adra kwa jicho pana zaidi, watakuwa wamegusa maisha ya wokovu kwa elimu hususani watoto wenye ualbino kwani moja ya sehemu nyengine ya mwisho ya mradi huo ni kuwa na mfuko wa uwezeshaji wa watoto wenye ualbino shuleni.
Mfuko huu wezeshi utakuwa ni msaada sana kwa watoto wenye ualbino kwani zile changamoto ambazo zinawakumba watoto wenye ualbino za gharama za mahitaji ya shule watakuwa wameenda kutibu kidonda cha wazazi ambao wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za elimu kama vile mavazi, madaftari n.k.
Post a Comment