WAJASIRIAMALI WA KIKE KILAKALA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI YA BIDHAA ZAO.
Diwani Mhe. Mwanaidi Ngulungu, akizungumza na wanawake Wajasiriamali.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kilakala, Delfina Pacho, akizungumza na Wanawake Wajasiriamali.
WANAWAKE Wajasiriamali Kata ya Kilakala wametakiwa kuongeza thamani bidhaa wanazozizalisha pamoja na kuboresha vifungashio ,ili kuhimili ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Diwani
wa Viti Maalum Manispaa ya Morogoro anayetokana na Kata ya Kilakala, Mhe.
Mwanaidi Ngulungu, katika kikao cha kuwachagua viongozi wa mpito na uundwaji wa Jukwaa la Wanawake Kata ya
Kilakala hivi karibuni.
Akizungumza na Wajasiriamali
hao wakike, Mhe.Ngulungu, amesema kuwa bidhaa za wajasiliamali zinaweza kupata
soko kubwa iwapo
zitaongezwa thamani na kufungashwa vizuri .
Mhe. Ngulungu, amesema
kuwa baada ya Jukwaa hilo kuznduliwa wataanzisha semina ya vikundi na
wajasiriamali ili kuweza kuwapatia elimu ya masoko na jinsi
ya kupanga bajeti.
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kilakala, Delfina Pacho, amesema mchakato wa kuwapata viongozi wa kikatiba utafanyika baadae kwani kwa sasa wamefanya uchaguzi wa mpito ili kuweza kupata Jukwaa hilo la Wanawake Kata ya Kilakala.
Kwa upande wa
Mjasiriamali maarufu Manispaa ya Morogoro, Lilian maarufu kwa jina la biashara
Lilian Catering, anayejihusisha na usambazaji wa chakula, amempongeza Diwani
Ngulungu kwa kuwakutanisha wanawake pamoja na kuahidi kushirikiana nao katika
kufikia malengo yao.
Post a Comment