MBUNGE MZERU ATIMIZA AHADI, AKABIDHI MIFUKO 100 SHULE YA SEKONDARI LUPANGA, MANISPAA YATOA NENO.
Katibu wa Mbunge Norah Mzeru (wapili kushoto) akikabidhi mifuko ya Saruji kwa niaba ya Mbunge Mhe. Norah Mzeru, (kushoto) Diwani wa Kata ya Kilakala Mhe. Marco Kanga, (wapili kulia ) Afisa Elimu Taaluma Sekondari Manispaa ya Morogoro, Mhaiki Deogradias, (kulia) , (kulia) Mkuu wa Shule ya Sekondari Lupanga, Flora Ndunguru.
Afisa Elimu Taaluma Sekondari Manispaa ya Morogoro, Mhaiki Deogradias, akimpongeza Mhe. Norah Mzeru.
Diwani wa Kata ya Kilakala Mhe. Marco Kanga.
Mifuko ya Saruji iliyotolewa na Mhe. Mzeru.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Lupanga.
Madarasa ambayo yamepewa saruji kwa ajili ya kukarabati.
Muonekano wa ndani wa Darasa madarasa mapya ya UVIKO-19 katika Shule ya Sekondari Lupanga.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mhe. Norah Mzeru, ametimiza ahadi yake ya kukabidhi Mifuko 100 ya Saruji Shule ya Sekondari Lupanga iliyopo Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ambayo yameonekana kuchakaa ili yaendane na madarasa mapya.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Mzeru, Katibu wa Mbunge huyo , Ismail Kifaru, amesema kuwa mifuko aliyotoa Mhe. Mzeru ametumia fedha zake binafsi kununua mifuko hiyo lengo likiwa ni kusaidia kufanikisha ukarabati wa madarasa ambayo yameonekana kuchakaa ili yaendane na madarasa mapya na wanafunzi wasome katika mazingira rafiki yenye kuvutia.
Kifaru, amewataka wanafunzi wa shule ya Lupanga kusoma kwa bidiii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kwamba atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazo wakabili kwa kadri atakavyoweza kujaliwa.
Katika hatua nyengine, Kifaru, amewapongeza wanafunzi waliofanya vizuri pamoja na kushakuru waalimu kwa kujitoa kwao katika kufundisha na kuongeza ufaulu shuleni hapo.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Afisa Taaluma Sekondari Manispaa ya Morogoro, Mhaiki Deograsias , amempongeza Mhe. Mzeru kwa mifuko hiyo ya saruji na kumuahidi mifuko hiyo itaenda kufanya kazi tarajiwa.
Naye Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amemshukuru Mhe. Mzeru na huku akisema kuwa kitendo cha Mhe. mzeru kutoa mifuko hiyo ya saruji kinaonesha ni jinsi gani Mhe. Mzeru anaunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassani ya kujenga miundo mbinu bora ya elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma bila shida.
Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Lupanga, Flora Ndunguru, amesema kuwa Msaada huo utasaidia kutatua changamoto waliyo nayo ya uchakavu wa madarasa .
Amesema wanatarajia kupokea wanafunzi 274 , hivyo kwa madarasa ambayo watayakarabati basi yatasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022.
Kwa upande wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza aliye jitambulisha kwa jina la Theresia Minja, ametoa pongezei kwa Rais Samia na kumshukuru Mbunge Mzeru , kwa moyo alio onyesha kujitoa kuwasaidia kutatua changamoto hiyo na kumuahidi kuwa watasoma kwa bidii naKufaulu kwa asilimia 100 katika mitihani yao pamoja na kuongeza ufaulu shuleni hapo.
Ikumbukwe ahadi ya Mhe. Mzeru, ya kutoa mifuko hiyo 100 ya Saruji, ilitokana na ziara yake ya kikazi aliyoifanya Januari 17/2022 katika kutembelea madarasa mapya yaliyojengwa na fedha za Maendeleo na ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 .
Post a Comment