Header Ads

DC MSANDO APIGA MARUFUKU UCHEPUSHAJI WA MAJI KATIKA VYANZO VYA MAJI


Mkuu wa Wilaya akiwa katika ziara ya kukagua vyanzo vya maji.

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amepiga marufuku suala la uchepushaji wa maji katika vyanzo vya maji.

Kauli hiyo, ameitoa hivi karibuni, katika ziara yake ya kukagua vyanzo vya maji pamoja na mtambo unaosambaza maji uliopo eneo la Tumbaku Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Msando, amesema kumekuwa na uharibifu  mkubwa wa vyanzo vya maji vinavyofanywa na wananchi kwa kuchepusha maji kutoka vyanzo vya maji.

Amesema kuwa wananchi wote ambao wamekuwa na tabia ya kuchepusha maji watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo faini pamoja na kifungo.

Aidha, DC Msando, amesema tayari katika Wilaya yake ameshaunda, kamati ya kufanya tathmini hiyo ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa na maji yanayopatikana yakawezeshe bwawa Mindu,  kwa ajili ya kuzalisha maji na wananchi kupata maji kwa uhakika.

Katika hatua nyenge, DC Msando,  amesema kuwa , Tanzania  imeamua kutumia uchumi wa viwanda ili kutekeleza azma ya Serikali kuelekea uchumi wa pato la kati, hivyo hata upandaji miti na maliasili ya misitu inaendana na uchumi wa viwanda.

DC Msando, kila mwananchi kuhakikisha anakuwa msimamzi wa mazingira na anatunza vyanzo vya maji kwa kufuata sheria na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na maji safi na salama kama haki ya msingi.

Naye, Mkurugenzi wa MORUWASA, Eng. Tamimu Katakweba, ametaka  elimu kwa wananchi iendelee kutolewa hususani ya kufanya shughuli za kiuchumi kando au pembezoni mwa mwa mito na vyanzo vya maji ili kutoathiri upatikanaji wa maji.

Kwa upande wa  Mhandisi wa rasilimali za Maji, Bonde la  Maji la Wami Ruvu ,akimwakilisha Mkurugenzi wa Bonde la Wami, John Kasambili,  amewataka wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kulinda miundombinu ya maji kwa kuwa wanaohujumu miundombinu hiyo wanafahamika kwakuwa wanaishi katika mazingira yao na pengine ni ndugu zao.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.