Header Ads

MBUNGE MZERU AFURAHISHWA NA UBORA MADARASA YA UVIKO-19 MANISPAA YA MOROGORO.



Madarasa mapya ya UVIKO-19 Shule ya Sekondari Lupanga.

Muonekano wa ndani wa Madarasa mapya ya UVIKO-19 Shule ya Sekondari Lupanga.


Mhe. Mzeru, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari , Lupanga.

Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Lupanga.

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupanga.

Wanafunzi wakiwa wameshawasili madarasa mapya ya UVIKO-19 Shule ya Sekondari Lupanga Kata ya Kilakala.

                

Diwani Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Shule Lupanga, Flora Ndunguru (katikati), pamoja na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru (kulia).

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia Chama Cha  Mapinduzi CCM ,Mhe. Norah Mzeru,  amefurahishwa na ujenzi wa madarasa ya UVIKO-19 Manispaa ya Morogoro katika.

Hayo ameyasema leo Januari 17/2022 wakati wa ziara yake ya kukagua madarasa hayo ambapo alianza na Shule ya Sekondari Mzumbe iliyopo Wilaya ya Mvomero iliyoingia katika nafasi ya 10 Kitaifa katika matokeo ya Kidato cha nne ya mwaka 2021.

Akizungumza mara baada ya ziara yake katika shule hiyo, Mhe. Mzeru amesema ,fedha hizo zilizotolewa na Rais Samia Suluhu, zinapaswa kuacha alama chanya kwenye sekta ya elimu, hivyo madarasa hayo lazima yawe ya mfano kama walivyofanya Manispaa ya Morogoro.

"Kwa mfano huu ambao nimeuona hapa shule ya Sekondari Lupanga naamini Madarasa yote yapo aina moja, kwa kweli ujenzi wa Viwango na unaridhisha sana na thamani ya fedha imeonekana,  nawapongezeni nyote ikiwamo Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Kaka yangu Abood,  Baraza la Madiwani chini ya  Mstahiki meya, Mkurugenzi wa Manispaa na Menejimenti yake, Wakuu wa Idara na Vitengo,  Wakuu wa Shule , Watendaji  na wengine wote, kazi ni nzuri. endeleeni hivyo hivyo”Amesema Mhe. Mzeru.

Aidha, Mhe. Mzeru, amesema  kuwa wanafunzi wote kwa mara ya kwanza historia ya Tanzania  inaandikwa, wameanza shule kwa siku moja tofauti na miaka ya nyuma ambayo kulikuwa na machaguo (selection) kutokan a na uhaba wa madarasa shuleni.

“Wananchi wa Mkoa wa Morogoro, tumpongeze Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba  hivi vya madarasa, ambapo watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza wameanza kusoma vizuri, nimeona mpangilio mzuri wa darasani , naamini kwa staili hii  watasoma katika mazingira mazuri sababu vyumba vya madarasa vipo vya kutosha lakini ufaulu pia utaongezeka" Amesema Mhe. Mzeru.
 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.