Header Ads

MANISPAA YAKAMILISHA UJENZI WA VIBADNA 88 VYA WAJASIRIAMALI ENEO LA FIRE.

 

Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu (katikati),akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana (kulia), (kushoto ) Mwanasheria Manispaa ya Morogoro, Elikarimu Teah wakati wa ziara ya kutembelea vibanda vya wajasiriamali.

Muonekano wa Vibanda vya wafanyabiashara wadogowadogo Mtaa mfupi eneo la Fire.

MANISPAA ya Morogoro imekamilisha ujenzi wa Vibanda 88 kati ya vibanda 150 vinavyotakiwa kujengwa katika eneo la Fire Mtaa Mfupi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro , Eng. Juma Gwisu, leo Januari 25/2022 katika ziara ya Kamati ya fedha ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza katika ziara hiyo, Eng. Gwisu, amesema mpaka sasa wameshakamilisha jumla ya vibanda 88 kati ya vibanda 150 vilivyo katika mpango wa ujenzi.

Eng. Gwisu, amesema mara baada ya kukamilika kwa vibada hivyo, kutasaidia wajasiriamali wadogowadogo kufanya biashara zao katika mazingira rafiki.

“Mpaka sasa tumekeamilisha vibanda 88, lengo letu na mpango wetu ni kujenga vibanda 150, lakini tutahakikisha  tunakamilisha kwa wakati vibanda vilivyobakia ili wafanyabiashara waanze biashara na kufanya kazi katika mazingira rafiki” Amesema Eng. Gwisu.

Manispaa ya morogoro ni miongoni mwa Manispaa zilizofanya vizuri katika ujenzi wa vibanda vya machinga na kuwa Manispaa ya mfano ya kujifunza ujenzi wa wa vibanda hivyo kwa kutekeleza ujenzi wa vibanda vya machinga katika Soko Kuu la Chifu Kingalu.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.