Header Ads

USTAWI WA JAMII MANISPAA MOROGORO YAMKABIDHI MTOTO ALIYEIBIWA KWA MZAZI WAKE.

                  

Afisa Ustawi Judithi Mbelwa, (watatu kutoka kushoto) akimkabidhi Mtoto kwa mzazi ambaye mtoto wake aliibiwa na kupatikana .

                

              

         

USTAWI wa Jamii Manispaa ya Morogoro imefanikiwa kumkabidhi mtoto  aliyeibiwa kwa mzazi wake kwenye Makao ya Kulelea Watoto yatima Mgolole.

Tukio hilo la makabidhiano ya mtoto limefanyika Oktoba 19, 2020 kwenye Makao ya kulelea Watoto yatima Mgolole.

Akizungumza juu ya tukio hilo, Afisa Ustawi, Judith Mbelwa, amesema mtoto huyo amekabidhiwa kwa Mzazi wake akiwa na afya nzuri huku akiushukuru Uongozi wa Makao hayo, kwa jitihada za kuwalea watoto hao.

Tukio hilo la kuibiwa Mtoto huyo aliyekuwa na miezi  2 ,  lilitokea tarehe 05 Oktoba 2020  Mkoa wa Kigoma Kata ya Nguruka na kufanikiwa kupatikana Mkoa wa Morogoro Manispaa ya Morogoro siku ya Tarehe 9, Oktoba ambapo alihifadhiwa kwenye Makao hayo.



1 comment:

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.