MAWAKALA WA VYAMA VYA SIASA JIMBO LA MOROGORO MJINI WAAPISHWA.
Msimamizi wa Jimbo la Uchaguzi Morogoro Mjini , Sheilla Lukuba, akiwaapisha Mawakala wa Chama cha CHADEMA kwenye Ukumbi wa Chuo cha SUA Oktoba 21,2020.
Mawakala wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakila kiapo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini.
MSIMAMIZI wa Ucaguzi wa Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, Leo tarehe 21 oktoba, 2020 amewaapisha Mawakala wa vyama mbalimbali vya siasa vitakavyoshiriki zoezi la uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika oktoba, 2020.
Akiendesha zoezi Hilo,Lukuba, amewataka Mawakala hao kutunza Siri za Uchaguzi Kama walivyoapa kwenye viapo vyao pamoja na kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za Uchaguzi za mwaka 2020 ili zoezi hilo lifanyike kwa amani na utulivu.
"Ni haki ya kila chama cha siasa kinachoshiriki Uchaguzi kuwa na wakala, ila tambueni kuwa Kwa wakala atakayeshindwa kuzingatia kiapo hiki hatua za kisheri zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kulipa faini au kifungo au vyote kwa pamoja" Amesema Lukuba.
Aidha, Lukuba, ameendelea kuwaeleza mawakala hao kuwa, kuapa kiapo hicho ni utekelezaji wa kanuni ya 50(4) ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 43(4) ya kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa( uchaguzi wa madiwani) za mwaka 2020.
Post a Comment