Abood aibuka kidedea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini kwa jumla ya kura 171,349
Afisa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Pendo Chagu, akimkabidhi Mhe. Abdulaziz Abood, Hati ya Kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini leo Oktoba 29/2020 mara baada ya kusaini kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro mara baada ya kuibuka kidedea.
MATOKEO ya nafasi ya wagombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini, yametoka leo Oktoba 29/2020 Majira ya saa 12:30 Jioni huku ikishuhudiwa Mhe. Abdulazizi Abood ,akiendelea kutetea kiti chake mara baada ya kuibuka kidedea kwa jumla ya kura 171,347 , akifuatiwa na Mgombe wa Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mathew Minja aliyepata kura 14,139, wakati mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo Hussein Sheshe akipata kura 720 na mgombea wa Chama Cha Wananchi CUF Abeid Haroub akiwa na kura 562.
Katika Jimbo la Morogoro Mjini, waliojiandikisha ni 286840 ambapo idadi halisi ya waliopiga kura ni 188,039, huku kura halali zikiwa ni 186,770 na kura ambazo zilikataliwa ni 1, 269.
Aidha, msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, amesema Jimbo hilo lina Kata 29 ambapo kati ya Kata hizo , Kata 10 zilipitwa bila kupingwa wakati wa uteuzi huku Kata 19 zimeweza kuchukuliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM katika kinyang''anyiro cha Uchaguzi.
Vyama vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu katika nafasi za Ubunge na Madiwani Jimbo la Morogoro Mjini, ni pamoja na CCM, CHADEMA, CUF na ACT WAZALENDO.
Post a Comment