Header Ads

KAMATI YA AMANI NA MARIDHIANAO MKOA WA MOROGORO YATOA TAMKO JUU YA UCHAGUZI MKUU.




Kamati ya amani na maridhiano Mkoani Morogoro imewataka watanzania  kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuepuka madhara mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na umwagaji damu.

Hayo yamebanishwa hivi karibuni na Kamati hiyo, wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa  Morogoro Hotel  iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo wamewataka wananchi kulinda amani waliyonayo kwa maslahi ya nchi na vizazi vijavyo.

Akiwa katika kikao hicho  Askofu Jacob  Mameo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema uwepo wa amani ndio unaopelekea watanzania  kuendelea kushiriki katika kazi mbalimbali bila woga ikiwa ni pamaja na kushiriki kwenda kwenye nyumba za ibada.

Hivyo, kukosekana kwa amani kutapelekea watanzania kutojihusisha na shughuli za kijamii na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kukosa utulivu kama baadhi ya nchi nyingine zilivopoteza amani na matokeo yake kuwa na vita visivyo na kikomo.

Ahmad Khailallah ambaye ni Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Morogoro amesema kwa upande wa Waumini wa dini hiyo hawana mgombea yeyote wa kiti cha urais ambaye waumini hao wanatarajia kumpigia kura kuwa Rais isipokuwa kila muumini atampigia kura Mgombea anayemtaka kulingana na sera alizotoa wakati wa kujinadi

“kama waislam hatuna mgombea ambaye tumemsema na kumtangaza ndiye atakayekuwa anasimamia Waislam, hatuna. mgombea wa Waislamu hatuna,  ila kila mtu anamgombea ambaye anajua nani ataenda kumpigia kura”alisema Khailallah.

Naye Askofu Dr. Peter Denis wa Kanisa la CPCT amewashauri vijana kutoshawishika kirahisi na wanasiasa ambao baadhi yao wanataka mara baada ya matokeo kutangazwa waingie mitaani na kufanya fujo jambo ambalo linaweza kuleta hasara kwao, akinamama, watoto na wazee.

Hata hivyo, Lawrence Mdee amewataka wanasiasa Kutumia busara zaidi na mazungumzo baina yao kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii na kuepuka kutumia silaha  dhidi ya wananchi  ili kunusuru taifa hili.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.