Header Ads

WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGUZI JIMBO LA MOROGORO MJINI WAHIMIZWA KUSIMAMIA ZOEZI KIKAMILIFU

                                       

Msimamizi msaidizi wa Jimbo la Uchaguzi Morogoro Mjini, Chausiku Masegenya, akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura Jimbo la Morogoro Mjini kwenye Ukumbi wa Mount Uluguru Manispaa ya Morogoro.

       

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, (kulia) akitoa maelekezo kwa Afisa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro Pendo Chagu (kushoto) pamoja na wasimamizi wa uchaguzi ngazi za Kata wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura.

                       

Mwanasheria wa Manispaa ya Morogoro, Wilfred Mramba, akiendelea na zoezi la viapo kwa wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura kwenye Ukumbi wa Mount Uluguru.

                                  









MSIMAMIZI msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro, Chausiku Masegenya,  amewataka Wasimamizi wa Vituo vya uchaguzi kusimamia zoezi hilo kikamilifu kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi .

Kauli hiyo, ameito leo Oktoba 25, 2020 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia kura kwenye Ukumbi wa Mount Uluguru Manispaa ya  Morogoro.

Masegenya , amesema pamoja na kwamba uzoefu ni nyenzo muhimu katika kufanikisha Uchaguzi lakini pia uzoefu unaweza kuwaponza kwa kufikiri kuwa wanajua kila kitu na kusahau kujisomea pamoja na kutozingatia  mafunzo waliyoyapata .

“Napenda kuwashukuru wote kwa ushirikiano mlioutoa wakati wa mafunzo mpaka tumemaliza kwa mafanikio,naamini malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa, lakini lazima mtambue kuwa  Tume imewaamini na kuwateua kuwa Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  , ikiwa na imani kuwa kazi hiyo mtaifanya kwa ufanisi ili kuwezesha Uchaguzi huu kufanyika kwa mafanikio makubwa, nipende kuwatakia safari njema ya kurejea katika maeneo na kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yenu ya Uchaguzi””Amesema Makupula.

Aidha, amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 74(6) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepew jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara.

“Katika kutekeleza jukumu hilo, Tume imekasimu madaraka kwa ngazi zifuatazo ikiwamo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo, Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo,  Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata , Wasimamizi wakuu wa vituo vya kupigia kura, Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura pamoja na Makarani Waongozaji wa vituo vya kupigia kura” Ameongeza Makupula.

Amesema mafunzo ya leo ni kwa ajili ya Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura, ambao ni watu muhimu katika zoezi hilo la Uchaguzi, kwani kufanikiwa au kutofanikiwa kwa zoezi kutategemea na utendaji wao katika vituo walivyopangiwa.

"Uchaguzi ni mchakato lazima mtambue kwamba zoezi hili linafanyika siku moja na nyinyi ndio watekelezaji wake, kama Tume inavyosisitiza kuwepo kwa uchaguzi huru na haki ambapo Tume inawategemea sana katika kutimiza malengo hayo"Amesema Masegenya . 


Hata hivyo, amewaomba wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia na kuyatambua vyema maeneo waliyopangiwa , ikiwemo miundominu na tabia za watu wa maeneo hayo kwa kuwa maeneo yanatofautiana.

Aidha, amewapongeza  Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata kwa michango waliyotoa wakati wote wa majadiliano na uzoefu waliobadilishana katika mafunzo hayo huku akisema uwepo wao katika kusimamia zoezi hilo umetoa mwanga na uelewa wa pamoja wa namna shughuli za uchaguzi zinavyoweza kuboreshwa wakati wote.

Mwisho ametoa wito kwa Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata kuendelea kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na Wataalamu wa afya kuhusu kujikinga na maambukizi dhidi ya Ugonjwa wa Corona (COVID-19.

 

 

 

 

 

 


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.