DC MSULWA AWAAMSHA WAIGIZAJI NA WASANII KURUDISHA HESHIMA YA MICHEZO WILAYA YA MOROGORO.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewata Wanamichezo na Wasanii waamke kwani huu ni muda muafaka wa kurudisha heshima ya Michezo katika Wilaya ya Morogoro.
Kauli hiyo ameitoa leo
Oktoba 02,2020 kwenye kikao cha kukutana na Wadau wa Michezo, Sanaa, Elimu na
Mazingira Manispaa ya Morogoro kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa kwa ajili
ya kujadili changamoto zinazozikumba sekta hizo.
Akizungumza na
Waandishi wa habari, DC Msulwa, amesema lazima Morogoro isimame na kurudisha
heshima yake katika Nyanja ya michezo, sanaa na utamaduni .
Msulwa, amesema anataka
Morogoro ya Viwango katika michezo hivyo ni ngumu kuipata Morogoro ya Viwangoi
kama huwezi kujua changamoto zake za kuanzia.
“Hiki ni kikao muhimu sana, tunahitaji kurudisha heshima ya Morogoro katika Sanaa na Michezo, tunaamini Morogoro ina vipaji vingi sana na asilimia kubwa ya wachezaji wametoka Morogoro , tulikuwa na timuz nzuri sana klakini leo tumebakiwa na timu moja Mtibwa Sugar lazima tujiulize ni wapi tumekosea ili tuanze na hapo, tunaamini tukishirikiana kwa pamoja Morogoro ya Viwango inawezekana”” Amesema DC Msulwa.
Mwisho. Amechukua nafasi ya kuwakaribisha Wanamichezo wote , Wananchi, Vikundi vya Michezo ikiwamo jogging, Watumishi wa Umma na binafsi katika Mkutano wa kujadili changamotoz a Wanamichezo na Wasanii ambapo kabla ya mkutano huo kutakua na mbio fupi zitakazooongozwa na Jogging kuanzia mishale ya saa 12:30 asubuhi kwenye Viwnaja vya Shule ya Msingi Mwere hadi Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Jamhuri ambapo Mkutano huo utafanyika .
Kwa upande wa Msanii wa filamu na maigizo , Haviti Makoti, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Morogoro huku akisema mpango aliouanzisha unalenga kuwajengea uwezo wasanii pamoja na Wananmichezo ili kutengeneza ajira kupitia tasnia ya filamu na michezo kwa ujumla.
Aidha, Makoti, amesema kuwa Wasanii wengi wa
filamu Morogoro wamekuwa wakicheza filamu zao nje ya Morogoro na kwenda Jijini
Dar Es Salaam, kutokana na Morogoro kuwa na shida ya kukuza vipaji vya sanaa
jambo ambalo limekuwa likidumaza sanaa za waigizaji hao kutofikia malengo.
Hivyo, kwa niaba ya
wasanii wenzake ,wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwaongezea nguvu ikiwamo kutafuta wadau ili
waweze kusaidiwa kazi zao za sanaa katika kukuza vipaji na kujipatia kipato
kama njia moja wapo ya ajira na kujikomboa na umasikini.
Kwa upande wa
mchangiaji , Kitutu Mshana, ameshauri kuwepo na
Makongamano ya kimichezo na sanaa ambayo yatawajumuisha Wanamichezo wote
wanaotokea Morogoro pamoja na wasaanii ili fedha zinazopatikana ziende kusaidia kuchangia huduma shuleni ikiwamo vitabu na madawati n.k.
Kitutu ,amesema ili
michezo iwe endelevu haipaswi ikawa siku moja pekee ipo haja ya watumishi
kukutani mishale ya jioni kufanya mazoezi ambapo kupitia wao wanaweza kukutana
na kujadili masuala mbalimbali ikiwamo kuanzisha michango mbalimbali
itakayoweza kusaidia kunyanyua michezo na sanaa katika Wilaya ya Morogoro.
Naye msanii Mwasity
Juma, amemuomba Mkuu wa Wilaya kuweza kusapati michezo hususani katika suala
zima la mitaji kwani wana uwezo wa kuandaa mipango mizuri ya kisanii kama
matamasha lakini changamoto inakuwa ni ukosefu wa fedha za kutangaza matamasha
hayo.
Post a Comment