Header Ads

WANANCHI MANISPAA YA MOROGORO WAOMBA AMANI ITAWALE BAADA YA MATOKEO.

 

WANANCHI wa Manispaa ya Morogoro wameomba amani itawale baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu kutangazwa  na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti leo Oktoba 31/2020, wamesema kilichobakia kwa sasa ni Wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuangalia mbele na sio  wakati wa kuzungumza siasa tena.

Kwa upande wa Zahara Ally, ambaye pia ni Mjasiriamali  kwa upande wa mama lishe ,amesema kuwa ni wakati wa Wananchi kufanya kazi, muda wa kampeni umeisha hivyo kila mtu ana wajibu wa kulinda amani na kuhakikisha kwamba maisha ya watu yasiingizwe na machafuko ya amani .

“”Uchaguzi umeisha, suala lililobakia ni kila mwananchi kulinda amani , tulikuwa katika Kampeni zimemalizika tunatakiwa kufanya kazi na kutojihusisha na vikundi ambavyo vina nia ovu na Taifa hili, tukubaliane na matokeo , Wananchi wameshaamua kuwachagua viongozi wanaowataka ,kikubwa tuwape ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo  yetu” Amesema Zahara.

Katika hatua nyengine, Athumani Ismaili, amesema zoezi la Uchaguzi liliendeshwa kwa uhuru na haki, kwani hata kwenye vituo vya kupigia kura walipokelewa vizuri na kuoneshwa ushirikiano mkubwa na Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura na hata vituo vilifunguliwa kwa muda sahihi uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi..

“Uchaguzi ulikuwa huru na haki, niwaombe wananchi wenzangu, lazima tuheshimu maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, tulianza na Kampeni , kasha wananchi waliwasikiliza wagombea wa vyama vyote  vya Siasa na kufanya maamzuzi, sasa wale wanaokataa na kuyapinga matokeo wanapata wapi ujasiri huo? Tusitumike ndugu zangu  tuangalie maisha yetu , familia zetu na kazi zetu, uchaguzi umeisha tunachohitaji amani iendelee kudumishwa hapa nchini na tuwape ushirikianao viongozi wetu walioshinda ili wafanye kazi zao, walisema tuwape kazi watutumikie kazi tumeshawapa tunasubiria maendeleo” Amesema Athumani.

Naye mfanyabishara ndogondogo maarufu kama mmachinga, Dotto Evarist, amewataka Vijana na makundi mbalimbali kutotumika hususani katika kipindi hiki ambacho baadhi ya Wanasiasa wasio na uzalendo kwa Taifa lao kutaka kuvuruga amani hapa nchini.

“”Niseme kuwa siasa ni kam mpira wa miguu, sio kila aingiae uwanjani ana kadi za  timu, ukiwaambia waoneshe kadi zao ni wachache watakuwa nazo wengi watakuwa washabiki tu, na ndio kama ilivyokuwa katika Kampeni, hivyo wakati huu sio wa maandamano ni wakati wa kufanya kazi na tukumbuke kuna maisha  baada ya uchaguzi, wazazi, ndugu na familia tuwe makini sana na wanasiasa ambao hawana uzalendo wa Taifa hili, wenzetu nchi za jirani na mataifa ya nje wameingia katika mkumbo huo wa maandamano sasa wanatapatapa, tufanyeni kazi tukisubiria mika 5 mengine ya uchaguzi “ Ameongeza Dotto.

 

 

 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.