Tangazo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala juu ya ziara ya Waziri wa Ardhi Mh: William Lukuvi
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala inawatangazia Wananchi wake wa Wilaya ya Ilala ziara ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi DESEMBA 17 saa 09 :00 asubuhi eneo la Gongolamboto Viwanja vya Kampala.
DC ILALA SOPHIA MJEMA amewataka Wananchi wote wenye migogoro ya Ardhi wajitokeze siku hiyo waje na vielelezo vyao WAZIRI wa Ardhi atasikiliza Kero za Wana Ilala wote zinazohusina na masuala ya Ardhi.
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA ILALA
DESEMBA 12/2018
Post a Comment