DC Mjema awataka wakina mama waumini wa Kanisa la Moravian Tabata Liwiti kujiunga na Jukwaa ili kuwezeshwa kiuchumi.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amewataka waumini wa wakina mama katika Kanisa la Moravian Tabata Liwiti kujiunga na Jukwaa ili kunufaika na mikopo inayotolewa Manispaa.
Hayo ameyasema leo wakati wa kuendesha harambee ya uchangiaji wa huduma za Kanisa kutoka kwa waumini.
Amesema kuwa , wakina mama hao wakiwezeshwa hata Kanisa hilo litafika mbali. Mbali na wanawake, hakuwaacha wakina baba huku akiwataka nao kujiunga na mifuko mbali mbali ya uwezeshaji ikiwamo Mfuko wa Madini pamoja na Uvuvi.
Wakati huo huo amempongeza Kamati ya Maendeleo ya Kanisa kwa kufanikisha ununuzi wa Gari kwa ajili ya kutoa huduma za kusafiri kwa Mchungaji wao katika kuwafikia waumini pamoja na shughuli nyingine za kijamii zinazohusiana na Kanisa hilo.
" Kwanza nitoa pongezi kubwa kwa Kamati yenu ya Maendeleo, kwani mmefanya kitu kikubwa sana kuhakikisha Mchungaji wenu hapati shida katika usafiri, hivyo ni mategemeo yangu gari hiyo itatumika vizuri na itakuwa kwenye uangalizi mzuri" Amesema DC Mjema.
Kuhusu changamoto ya Uzio wa Kanisa, DC Mjema amesema yupo tayari kuwaaaidia ili kuweza kuweka hali ya kiusalama katika kuepusha migogoro na majirani pamoja na kuzuia uharifu. Amesema Ofisi yake katika kuona hilo linafanikiwa, ameahidi kutoa mifuko 50 ya Saruji.
Hata hivyo amewaahidi kuwapatia ufumbuzi wa hati za maeneo mwezi januari ili maeneo yote yanayomilikiwa na Kanisa hilo yawe na vibali vinavyoonesha umiliki wao. Hivyo ameiomba Kamati ya ujenzi ifike ofisini kwake kwa ajili ya kutatua hayo mambo.
Amesema Kata ya Liwiti ni miongoni Mwa eneo ambalo lina changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi, hivyo atahakikisha inamalizika baada ya ziara ya Waziri wa Ardhi, Mh: William Lukuvi, kufanya ziara yake.
Amesema hati kwa sasa upatikanaji wake ni rahisi haichukui mudarefu ni kiasi cha wiki mbili zoezi limekwisha.
Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Jackson Mbaruku, amesema Kanisa hilo lilianza na waumini wa Kikristo 12 mwaka 1998 Februari hadi kufikia waumini 600 mwaka huu 2018 ambapo waumini hao ndio walifanikisha hatua za ujenzi.
Aidha Mchungaji huyo, amesema Kanisa hilo lina miradi mbali mbali ikiwamo Shule za Chekechea, Msingi, Saccos, Zahanati , kituo cha kulelea watoto , hosteli pamoja na kumbi za mikutano.
Amesema dhumuni la uanzishwaji wa Kanisa hilo ni pamoja na kumwendeleza mwanadamu kiroho, kumsaidia mwanadamu kuhimili maisha bila uovu.
Pia amesema kwenye madhimuni lazima mafanikio yawepo ambapo miongoni Mwa mafanikio hayo ni pamoja na kujenga jengo la Kanisa hilo lenye thamani ya Pesa za Kitanzania, Shilingi Milioni 4 na laki 2, Jengo la Mchungaji Milioni 160, kuongeza kazi ya uinjiristi kutoka waumini 12 hadi 600, kusaidia wajane, yatima, na watoto wanaoishi katika Mazingira magumu pamoja na kutatua migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Kanisa hilo.
Hata hivyo amesema Kanisa hilo licha ya kuwa na mafanikio lakini linakabiriwa na changamoto kama vile, ucheleweshwaji wa kumilikishwa maeneo yaliyo mbele ya Kanisa hilo tangia wafuatilie mwaka 2015 mpaka Leo hakuna majibu hivyo DC Mjema kasema swala hilo lipo ndani ya uwezo wake atalifanyia kazi.
Pia suala la wigo wa Kanisa ili kuepuka miingiliano isiyo ya kilazima na majirani ambapo uzio huo uta gharimu Shilingi Milioni 100 huku akisema changamoto nyingine za Kanisa watatatua wenyewe.
DC Mjema mbali na ushiriki wake, amepata wasaa wa kufanya harambee ya kuchangia mafuta ya gari la Mchungaji na Pesa ya kukamilisha leseni ya gari ambapo kila mmoja alishiriki kwa kutoa Pesa hiyo kununua kipande cha Keki.
Pia kuliambatana na ugawaji wa vyeti kwa waumini waloioshoriki kikamilifu katika ujenzi wa Kanisa ma kujitoea kwake.
Post a Comment