TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Guru Planet inatarajia kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali mbalimbali.
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Guru Planet inatarajia kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali mbalimbali.
Mafunzo hayo yanatarajia kufanyika January Mwakani, yatashirikisha vijana wote wa Wilaya ya Ilala na mkoa wa Dar es Salam .
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salam leo Mkurugenzi wa Guru Planet Nicksoni Martin alisema mafunzo hayo yatakuwa ya mwezi mmoja, ngazi ya Ualimu kwa Wajasiriamali.
Pia mafunzo mengine yatakayotolewa yatahusisha watengezaji wa Sabuni,keki,usindikaji wa vyakula,mapambo na Mapishi.
"Guru Planet taasisi isiyo ya kiserikali ambayo ipo Manispaa ya Ilala inafanya shughuli zake kwa ajili ya kuwasaidia Wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao Halmashauri ya Ilala imetupatia kibali na tunatambulika kisheria" alisema Martin.
Martin alisema mafunzo mengine yatakayotolewa katika taasisi hiyo namna ya kuandaa mchanganuo wa biashara,mafunzo ya kompyuta.
Aidha alisema kundi la kwanza la watu 40 watakaofuzu mafunzo hayo watapewa ajira na taasisi hiyo ya Guru.
"Washiriki wote nawaomba mje chukua fomu Makao makuu ya Taasisi yetu kwa ajili ya usajili Tabata Wilayani Ilala "alisema
Post a Comment